Hivi punde: Sayyid Swafi akutana na viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) karibia na kuanza vita kwa ya Tal-afar, na asisitiza kua kumuokoa kiumbe ni bora kuliko kumuua gaidi..

Maoni katika picha
Alasiri ya Juma Nne (22 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (15 Agosti 2017m) kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amekutana na viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji karibia na kuanza kwa vita ya Tal-afar.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Qassim bun Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Zifuatazo ni pointi muhimu alizo waambia viongozi wa kikosi hicho:

  • 1- Tusidharau uwezo wa adui hata kama akionekana dhaifu kiasi gani, madamu kabeba siraha haifai kumdharau, unaweza kupata hasara ukifanya hivyo, mtu shujaa ni yule asiye dharau na anapambana na adui kwa umakini na tahadhari, na anafanya maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kushinda vita.
  • 2- Inatakiwa kikosi hiki kiwe na mafunzo ya hali ya juu na maandalizi mazuri pamoja na baadhi ya matatizo yaliyopo, mafunzo bora na mazoezi humfanya mtu kua imara, yapafa mpiganaji aendelee kujifunza wakati wote.
  • 3- Kushikamana na tabia za Ahlulbait (a.s), sisi ni watu wenye maadali mema, kua na maadili mema ni muhimu kwa sababu nyingi, miongoni mwa sababu hizo ni:



Sababu ya kwanza: Hakika vita hii, ni vita ya kihistoria kila kitu kitaandikwa, mambo muhimu yanayo takiwa kuandikwa ni maadili mema na kulinda uhai wa viumbe wasio husika kwa lolote katika vita, mara nyingi adui hufanya mambo ya kinyama yaliyo mbali na ushujaa pamoja na maadili mema, na huwafanya watu wasio kua na hatia kua ngao yake, hujifinya nyuma ya watu hao ili asishindwe, lakini mpiganaji shujaa ni yule asiye mbebesha mtu mwema makosa ya muovu, anatakiwa alinde roho za wanyonge, wale ambao maadui huwatumia kama ngao kwao, hivyo mpiganaji anajukumu lingine muhimu zaidi, nalo ni kulinda uhai wa viumbe wasio husika na vita.



Sababu ya pili: Hakika kuokoa kiumbe ni bora kuliko kumuua gaidi, mnatakiwa kizingatia hilo, lakini mnatakiwa kuwa makini sana katika kuchambua na kuwabaini wapiganaji na wasio kua wapiganaji.

  • 4- Tutavitaarifu vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu kua pamoja na nyie katika vita hii kadri watakavyo weza.
  • 5- Mnatakiwa kua na mawasiliano ya karibu pamoja na vikosi vyote vinavyo shiriki katika vita hii tena kwa kiwango cha juu kabisa na hili jambo ni muhimu sana.
  • 6- Tutahakikisha mafanikio kwa pamoja, masharti haya iwapo yakifatwa Mwenyezi Mungu ataleta ushindi wa haraka.



Tunapenda kukumbusha kua mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidiy alifanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Juma Tatu (21 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (14 Agosti 2017m) akasema kua, vikosi vitakavyo shiriki katika vita inayo tarajiwa kuanza hivi karibuni ya kukomboa mji wa Tal-afar ni:



Vikosi vinavyo fungamana na Hashdi Sha’abi chini ya kanuni namba (26).

Vikosi vinavyo fungamana na wizara ya ulinzi ya Iraq.

Vikosi vya hakiba miongini mwa vikosi vya Abbasi (a.s), ambao wameitwa kupitia wawakilishi wetu katika kila mkoa, wale walio fundishwa mbinu mbalimbali za kivita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: