Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chafanya kongamano la kwanza la kusaidia mujahidina wa Iraq..

Maoni katika picha
Jioni ya Alkhamisi ya (25 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (17 Agosti 2017m), kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya kongamano la kwanza chini ya kauli mbiu isemayo: (Vikundi vya kusaidia mujahidina ni washirika muhimu katika kuleta ushindi).

Kongamano hili liliendeshwa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na idadi kubwa ya wajumbe wa vikundi vya Husseiniyya kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq.

Kongamano hili linafanyika kwa ajili ya kuangalia changamoto wanazo kutana nazo wale wanaotaka kusaidia wapiganaji, wakati wa safari zao kuelekea katika maeneo wanako patikana wapiganaji wa kujitolea wanao tekeleza fatwa tukufu, pamoja na kuangalia namna ya kuunganisha nguvu katika vita ya Tal-afar.

Vikajadiliwa vikwazo mbalimbali pamoja na namna ya utatuzi wake chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekh Haitham Zaidiy, na Haji Riyaadh Ni’mah Salmaan rais wa vikundi vya Husseiniyya vya Iraq, na mwanachuoni wa kiislamu muwakilishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya).

Baada ya kusikiliza changamoto mbalimbali, Zaidiy alisisitiza kua: “Tumewaambia wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wawafanyie wepesi katika safari kwa kuwaondolea baadhi ya vizuizi vya barabarani hususan wakati wa usiku”. Pia akasisitiza ulazima wa misafara ya misaada kuheshimu maelekezo ya askari wa barabarani kwa ajili ya usalama wao, na akaahidi kua maombi mengine yaliyo juu ya uwezo wa kikosi cha Abbasi atayafikisha sehemu husika, na yatatafutiwa utatuzi wake inshallah, akaviomba vikundi vinavyo toa misaada kwa wapiganaji viwe vinawasiliana ili misaada yao isifanane.

Ukaelezewa umuhimu wa kusaidia vita ijayo ya kukomboa mji wa Tal-afar, kwa kuwapa mahitaji ya lazima wapiganaji wetu watukufu, pamoja na kuwasaidia wakimbizi wakati wa vita.

Rais wa vikundi vya Husseiniyya Haji Rifaadh Ni’mah katika ujumbe wake alisema kua: “Hakika watu wa Mosul wanakumbuka msimamo mtukufu ulio onyeshwa na vikundi vya Husseiniyya katika kusaidia wakimbizi, hususan baada ya wito wa Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu pale alipo sema, okoeni nafsi zenu na familia zenu katika mji wa Mosul kutokana na tabu ya njaa na kiu. Vikundi vya Husseiniyya vikajitokeza kwa wingi sana kupeleka misaada chini ya mashambulizi makali ya Daesh na mazingira magumu sana walihakikisha misaada inawafikia wanawake na watoto pamoja na wakimbizi wote, hivi ndio mnatakiwa kua enyi wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kuwafundisha walimengu ubinadamu na namna ya kuonyesha mapenzi kwa ndugu yako mwanadamu.

Akaongeza kusema kua: “Hii hapa vita ya Tal-afar imekaribia, yatupasa tuinuke enyi wazalendo tuwasaidie majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s), pamoja na vikosi vingine vyote vinavyo ingia katika vita hiyo, tuwape msaada wa hali na mali ndugu zetu wapiganaji watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: