Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu wahudhuria tukio la kubadilisha bendera za kubba za maimamu wawili Jawadaini (a.s) na kuwekwa bendera zinazo ashiria huzuni..

Maoni katika picha
Kuhuisha ahadi na utii kwa Mtume Mtukufu na watu wa nyumbani kwake watoharifu (a.s), ugeni unaowakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu umehudhuria tukio la kubadilisha bendera za kubba mbili tukufu za maimamu wawili Jawadaini (a.s), na kupandisha bendera zinazo ashiria huzuni kwa ajili ya kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Muhammad Jawaad (a.s), ukumbi wa haram tukufu ya Imam Kaadhim (a.s) jioni ya siku ya (25 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (18 Agosti 2017m) ulishuhudia tukio la kila mwaka la kubadilisha bendera za kubba bili tukufu za maimamu wawili Jawadaini (a.s) na kupandishwa kwa bendera zinazo ashiria huzuni.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na wawakilishi wa Ataba mbalimbali na mazaru wakiwemo walimu wa vyuo na hauza za kidini pamoja na idadi kubwa ya wanasiasa na viongozi wa kijamii, bila kuwasahau wanausalama na watumishi wa Jawadaini (a.s) na mazuwaru watukufu.

Shughuli ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha vikafuatia vikundi vya mawakibu vya mji wa Kadhimiyya vikaingia vikiwa vimenyanyua bendera za kuonyesha utiifu katika tukio hili liumizalo. Ukafuata ujumbe wa Atabatu Kadhimiyya tukufu ulio wasilishwa na katibu mkuu wa Ataba hiyo, ambaye alisema kua: “Leo tunahuisha hisia za huzuni na zinapepea bendera nyeusi zinazo ashiria huzuni juu ya vichwa vyetu, leo yametawala kwetu majonzi na simanzi ya kuuawa kwa Imamu Jawaad (a.s), aliye ijaza dunia elimu na ukarimu, hakika alikua ni alama kubwa ya uislamu duniani, lazima awe hivyo kwani yeye ni imamu mteule wa kuinua utukufu wa dini na kulinda mila za uislamu, aliwashangaza wanachuoni wakubwa katika zama zake kutokana na ukubwa wa elimu yake, walipo mfuata kwa mijadala ya kielimu, akawashinda katika kila fani hadi wakakiri kushindwa kwao na ukubwa wa elimu yake”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika Imamu Jawaad (a.s) hawezi kusahaulika kwa kifo chake, ataendelea kua mfano hai katika kila kizazi, na msiba wake utaombolezwa kila mwaka hususan na vijana wetu, kwani Imamu (a.s) alikufa akiwa katika umri wa ujana, na leo taifa letu linapitia wakati mgumu, linashambuliwa na magaidi wa Daesh kila kona, vijana wamesimama imara kulinda taifa lao na maeneo matakatifu”.

Baada ya ujumbe wa katibu mkuu bendera za kijani zikashushwa na kupandishwa bendera nyeusi zinazo ashiria huzuni, shughuli ikamaliziwa kwa Qaswida za maombolezo zilizo imbwa na mshairi Karaar Alkaadhimi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: