Mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa ni kimbilio la taasisi mbalimbali na wadau wa Qur’an wa kitaifa na kimataifa..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mirabi bora ya Qur’an inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ni mradi wa (kiongozi wa wasomaji wa kitaifa) kulea na kuandaa wasomi wa Qur’an nchini Iraq, unao simamiwa na kuendeshwa na kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur’an, chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, uzoefu wao umeleta mafanikio, kwa kuthibitihsa hilo! Wamekua kimbilio la taasisi mbalimbali na wadau wa Qur’an wa kitaifa na kimataifa, kwa ajili ya kukagua vipaji vya washiriki na kuangalia namna ya kuviingiza katika uwanja wa Qur’an, kwa kuwasaidia kihali na mali na kufungua milango ya kusaidiana katika nyanja za Qur’an.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa mradi huu wamesema kua wamesha pokea wageni mbalimbali wakiwemo:

  • 1- Ugeni kutoka taasisi ya Qur’an Thaqil Akbar kutoka Bagdad.
  • 2- Kituo cha Qur’an Rasul A’adham kutoka Basra.
  • 3- Majmaa Qur’an kutoka Dhiqaar.
  • 4- Taasisi ya Qur’aniyya Al-iraqiyya kutoka katika matawi yake mbalimbali ya Bagdad.
  • 5- Taasisi ya (Dhaati) ya elimu ya maendeleo kutoka Lebanon.
  • 6- Raabitwatu Qur’aniyya kutoka Basra.
  • 7- Kitengo cha Qur’an cha taasisi ya Shaheed Mihraab pamoja na taasisi kadhaa za Qur’an.
  • 8- Madrasat As-haabu Kisaa ya Qur’an.
  • 9- Jumuiya ya Alkitaabul-Mubiin ya maarifa ya Qur’an tukufu.
  • 10- Taasisi ya Hauraa (a.s) ya Qur’an kutoka Bagdad.

Huo ni ugeni rasmi ulio ongozwa na wakuu wa taasisi hizo, amma kuhusu wadau wa Qur’an, ofisi ya mradi huu imesha pokea watu wengi sana walio kuja kutembelea mradi, walipokua wakitembelea madarasa na vifaa vinavyo tumika kufundishia washiriki wa mradi huu, na baada ya kupata maelezo kutoka kwa wakufunzi, walionyesha furaha kubwa na wakapongeza sana kile walicho kiona na kusikia, na wakasema kua hakika huu ni mradi wa kwanza katika sekta ya Qur’an wa aina hii, fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Qur’an inamiradi mingi ya Qur’an tukufu na inafuata njia sahihi katika utekelezaji wa miradi yake na ndio maana mafanikio yake yameanza kuonekana.

Idara ya mradi wa (Kiongozi wa wasomaji wa kitaifa) imesema kua milango yake iko wazi kwa taasisi zote na kwa kila mtu mdau wa Qur’an anayetaka kuwatembelea katika siku za usoni, ilikurahisisha swala hilo unatakiwa kupiga simu siku moja kabla ya kuwatembelea kupitia namba ifuatayo (07801286978).

Tunapenda kukumbusha kua mradi huu unawalimu walio bobea katika masomo ya Qur’an kutoka ndani na nje ya nchi, unalenga kutengeneza kizazi bora cha wasomaji wa Qur’an wenye misingi madhubuti, wanaandaliwa vijana wadogo wenye vipawa vya Qur’an kwa kufuata njia za kisasa, wanasomeshwa mambo muhimu kwa muda mfupi, na walengwa wakuu wa mradi huu ni wanafunzi wa shule za msingi na upili (sekondari) kutoka mikoa yote ya Iraq, na hutumiwa muda wa likizo za majira ya joto (kiangazi) ambao ni miezi miwili takriban katika hatua ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: