Katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar: Kikosi cha Abbasi chasonga mbele kwa kasi huku makombora yake yakitua katika ngome za Daesh..

Maoni katika picha
Wapiganaji wa Abbasi (a.s) kikosi cha (26) wanasonga mbele kwa haraka katika vita ya (Tunakuja ewe Tal-afar) dhidi ya magaidi ya Daesh, kwa kushirikiana na jeshi la serikali kikosi cha (36) pamoja na vikosi vingine vya Hashdi Sha’abi wamefanikiwa kudhibiti barabara kuu inayo onganisha baina ya vitongoji vya Shekh Ibrahim, Mahlabiyya na Tal-afar.

Hali kadhalika wapiganaji wa Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na kikosi cha tisa cha jeshi la Iraq wamefanikiwa kudhibiti upande wa kusini wa milima ya Zambar na pembezoni mwake, ili baada ya hapo waelekee sehemu ya viwanda kaskazini ya mji wa Tal-afar.

Kwa upande mwingine kikosi cha mizinga cha Abbasi (a.s), kutokana na taarifa za kiupelelezi walizo nazo wamefanikiwa kushambulia ngome muhimu za magaidi ya Daesh katika kitongoji cha Hassan Kawe ndani ya mji wa Tal-afar, kwa mujibu wa taarifa za kipelelezi, mashambulizi hayo yamefanikisha kuua idadi kumwa ya magaidi ya Daesh miongoni mwao ni kiongozi wao aitwaye (Abuu Yusufu Ruusiy) pamoja na (Abuu Yunis Al-Adhariy) ambaye ni kamanda mkuu wa magaidi katika mji wa Tal-afar, vile vile wameangamiza kituo cha mawasiliano cha Daesh na kuuliwa kwa gaidi lingine liitwalo Sudi Qublani, pamoja na kuangamiza kituo cha kuhifadhi vifaa vya kijeshi.

Huu ni muhtasari wa taarifa tulizo zipata kutoka katika uwanja wa vita, mapambano bado yanaendelea, tutaendelea kuwapa taarifa kadri zitakavyo tufikia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: