Kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chatoa kitabu cha (Mwenendo wa haki, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu) na chasisitiza kua ni kitabu muhimu katika maktaba za kiislam..

Maoni katika picha
Miongoni mwa machapisho yake ya kitaalamu, kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya wametoa kitabu cha (Mwenendo wa haki, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu) ni kitabu chenye maelezo ya ujumla, kinahitaji ufafanuzi kwa mtu aseyekua na elimu kubwa, kwani hataweza kufahamu kwa undani yaliyo andikwa atahitaji kufafanuliwa na kupewa mifano.

Mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau-dini Aali Maajid Zubaidi, amesema kua: “Kitabu kimeandikwa na Muheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Halo (d.b), nacho ni muongozo kwa anayetaka kufuata njia sahihi ya kujifundisha maarifa ya Qur’an tukufu na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) na kinafafanua uhusiano uliopo baina ya Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu kama ilivyo thibitishwa na hadithi tukufu ya vizito viwili”.

Akaendelea kusema kua: “Kupitia kitabu hiki tumemuweka Mtume Muhammad (s.a.w.w) sehemu nyeupe na katika njia safi, ili macho yasikose kumuona na miguu isishindwe kumfuata, baada ya hoja za wazi kutoka katika Qur’an tukufu na hadithi za maimamu watakasifu, zilizopo katika kitabu hiki, zinazo fafanua hatithi ya vizito viwili kisha kuifafanua Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu pamoja na namna ya kuzifanyia kazi aya za Qur’an na riwaya za Maimamu kwa maelezo mafupi na yenye kueleweka”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kitabu hiki katika toleo la kwanza kina kurasa karibu (275), hivi sasa kimewekwa katika maonesho ya vitabu vya Maahadi ya Qur’an tukufu, mkabala na mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya Tukufu, tunakusudia kukipeleka katika vyuo vikuu vya Iraq na ofisi za usambazaji wa vitabu za Bagdad pamoja na mikoa mingine ya Iraq, hatimae kukisambaza katika nchi zingine duniani inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: