Mwishoni mwa mwezi wa Dhulqa’adah aliuawa kishahidi Imamu Jawaadi (a.s)..

Maoni katika picha
Mwishoni mwa mwezi wa Dhulqa’adah mwaka (220m), aliuawa kishahidi Imamu Jawaad (a.s) kwa sumu iliyo toka kwa Mu’taswimu Abbasiy, Jafar bun Ma-amun aliwasiliana na dada yake Ummul-Fadhil mke wa Imamu Jawaad (a.s), Mu’taswimu alikusudia kumuua Imamu bila kujali utukufu wa Mtume (s.a.w.w), na sababu pekee iliyo mpelekea kufanya jambo hilo ni husuda dhidi ya Imamu (a.s), kwani likua anaheshimiwa sana na waislamu wote.

Akamrubuni mwanaye na kumuelekeza namna ya kumuangamiza Abuu Jafari (a.s) kwa kumuwekea sumu kali katika chakula, naye akachukua sumu ile na akaenda kumuwekea Imamu (a.s) katika chakula.

Imamu alipo kula chakula chenye sumu alihisi maumivu makali sana, Ummul-Fadhil alijutia sana kitende alicho fanya, akaanza kulia kwa uchungu, Imamu akamuambia: Mwenyezi Mungu atakuadhibu kwa ufakiri na atakupa balaa. Akapewa mtihani wa maradhi, akatumia mali zake zote katika matibabu hadi zikaisha na akawa fakiri mkubwa, na kaka yake Jafari (mtoto wa Mu’taswimu) alianguka ndani ya kisima kirefu, akatolewa humo akiwa amekwisha fariki.

Imamu (a.s) alifariki kutokana na sumu kali aliyo kula akiwa na umri wa miaka 25.

Mwili wake mtukufu ukapelekwa kuzikwa katika makaburi ya Maquraishi, ukishindikizwa na watu lufufu (wengi sana) walio kua hawajawahi kushuhudiwa katika mji wa Bagdadi, mji mzima ulijaa simanzi na majonzi kwa kuondokewa na Imamu (a.s) huku wakizungumzia hasara kubwa iliyo upata umma wa kiislamu kwa kufariki Imamu (a.s).

Kaburi lake likachimbwa ubavuni mwa kaburi la babu yake Imamu Kadhim (a.s), mazishi yakasimamiwa na mtoto wake Imamu Ali Haadi (a.s) kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: