Ewe muulizaji wa nini kimejiri katika mji, kuna tukio la kuanguka kwa nguzo ya uongofu.
Nilimjibu dini imepoteza kipenzi chake, pindi aliposema Jibrilu kuhusu tukio la Jawaad.
Maukibu (kikundi) cha watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya Adhuhuri ya siku ya Juma Nne ya (29 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (22 Agosti 2017m) walitoka na kwenda kutoa taazia kwa Imamu Hussein na mjikuu wake Swahibu Asri wa Zamaan (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kufariki kwa imamu Muhammad Jawaad (a.s) aliye fariki siku kama ya leo.
Walisimama katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakaimba qaswida za kuomboleza, kisha wakaelekea katika haram ya imamu Hussein (a.s) wakiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na naibu wake pamoja na jopo kubwa la watumishi wa Ataba tukufu.
Walipo wasili katika haram tutufu waliwakuta watumishi wa haram hiyo wamesimama rasmi kuwapokea, wakaungana pamoja katika haram tukufu ya imamu Hussein (a.s) na wakafanya majlisi ya taazia, na kuonyesha utiifu wao kwa imamu wa tisa Muhammad Jawaad (a.s), na wakasema kua mnasaba huu ni sawa na taa linalo waangazia katika kuwahudumia mazuwaru (watu wanaokuja kutembelea) malalo haya matukufu.