Kikosi cha Abbasi pamoja na kikosi cha tisa cha jeshi la Iraq wamedhibiti mtaa wa kijani (Khadharaa) katika mji wa Tal-afar, na wamevunja ngome ya adui katika mtaa wa Nuru na Jazira..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na brugedi namba moja na mbili ya kikosi cha (36) cha jeshi la serikali, pamoja na kikosi cha tisa cha mizinga, wametangaza udhibiti kamili wa mtaa wa kijani (Khadharaa) upande wa mashariki ya Tal-afar, sasa hivi wanaendelea na kutegua mabomu ya kutegwa aridhini pamoja na vilipuzi vilivyo tegwa kila kona na magaidi ya Daesh kwa lengo la kutatiza usongaji mbele wa majeshi ya ukombozi.

Katika vita hii kikosi cha Abbasi (a.s) kimetumia wapiganaji wake wa hakiba, ambao wamepigana kwa ujasiri na ushujaa wa hali ya juu kabisa na kufanikiwa kuvunja ngome zote za magaidi ya Daesh, na wamewapa hasara kubwa ya mali na nafsi.

Majemedari hawa kwa kushirikiana na kikosi cha (36) na baada ya mashambulizi makali, wamefanikiwa kuvunja ngome ya adui na kuingia katika mtaa wa Nuru na Jazira.

Mafanikio yaliyo patikana ndani ya siku tatu toka kuanza kwa vita hii, yanatokana na mafunzo mazuri waliyo pata pamoja na roho ya ujasiri waliyo nayo, pia ni matunda ya mawasiliano mazuri yaliyopo baina yao na vikosi vingine vinavyo shiriki katika vita hii.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kimeshiriki katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, kikiwa na wapiganaji elfu tano, walio gawanywa katika brugedi tatu; ya mizinga, watembea kwa mikuu, na brugedi ya mikakati, katika hatua ya kwanza wamefikia malengo yao yote na wametoa kipigo kikali kwa adui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: