Kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chaendesha semina kuhusu mwenendo wa haki..

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha semina ya kwanza ya kujenga uwezo siku ya Juma Nne ya (29 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (22 Agosti 2017m).

Semina hiyo inahusu (Mwenendo wa haki na kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu), hilo ndilo jina la kitabu kilicho tolewa hivi karibuni na Maahadi ya Qur’an tukufu, na mkufunzi wa semina hii ni mwandishi wa kitabu hicho Shekh Dhiyaau-dini Aali Majidi Zubaidiy.

Shekh Zubaidiy aliongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu semina hiyo, akasema kua: “Semina itachukua siku tano, kila siku ina saa mbili za kukaa darasani, hii ni miongoni mwa semina muhimu sana kutokana na maudhui zake ambazo tunaelezea nukta muhimu zilizopo katika kitabu kilicho chapishwa hivi karibuni ambacho semina hii imebeba jina la kitabu hicho, tutafafanua yaliyomo ndani ya kitabu hicho pamoja na rejea zake, wanasemina wamepewa kitabu hicho ili wakisome na sehemu ambayo watahitaji ufafanuzu zaidi tutawapatia, washiriki wa semina hii wanaweza kua walimu wa kitabu hiki katika semina zijazo, wataweza kukifafanua vizuri kama watazingatia maelekezo wanayo pewa katika semina hii”.

Akaongeza kusema kua: “Tunafanya semina hii kutokana na umuhimu wa mwenendo wa haki, kwa sababu Mtume (s.a.w.w) alituachia njia sahihi ya kuifahamu Qur’an tukufu kwa kupitia mwenendo wa vizito viwili, Qur’an na kizazi kitakasifu, hivyo tunahitaji kufahamu kwa usahihi mwenendo huo, ili utuongoze katika elimu zote za kisheria na tuweze kutambua muandishi anayetuongoza katika njia sahihi, mtu anaeshiriki katika semina hii ataweza kubaini mwenendo wa haki na mienendo mingine".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: