Hivi punde: Ofisi ya Ayatullah Sayyid Sistani (d.dh.w) yatangaza kua kesho ni siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul-hijjah..

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyidi Ali Hussein Sistani (d.dh.w) imetangaza kua kesho siku ya Alkhamisi (24 Agosti 2017m) itakua siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Dhul-hijjah 1438h.

Kutokana na tangazo hili, siku ya kwanza ya sikukuu ya Iddi Adh-ha itakua Juma Mosi (10 Dhul-hijjah 1438h) sawa na (2 Septemba 2017m).

Kutokana na tangazo hili tukufu, mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa mkono wa pongezi, kwa umma wa kiislamu na Maraajii wetu watukufu pamoja na raia wote wa Iraq bila kuwasahau wafuasi wa Ahlulbait (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu akubali matendo yetu na matendo yenu, na awape neema ya amani wananchi wa Iraq, alinusuru jeshi letu tukufu pamoja na Hashdi Sha’abi takatifu, awape ushindi wa haraka dhidi ya adui wa dini na taifa, hakika Mwenyezi Mungu ni msikivu wa dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: