Hivi punde: Sayyid Swafi atuma ujumbe wa sauti kwa majemedari wa kikosi cha Abbasi, awathibitishia kua wamefurahishwa na ushindi wao..

Maoni katika picha
Kufuatia kuwepo kwake katika msitiri wa mbele wa vita ya Tal-afar siku ya pili mfululizo, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ametuma ujumbe wa sauti kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), akiwaambia kua:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi ndugu zangu watukufu na rehema zake na baraka zake..

Siku ya Ijumaa ya leo tukufu tunatoa pongezi kubwa sana kwa mafanikio mnayo endelea kupata, Mwenyezi Mungu akulipeni kila la kheri, mafanikio haya yataandikwa kwa nuru katika vitabu vya matendo yenu, na itabaki kua historia nzuri kwenu na kwa familia zenu tukufu, hali kadhalika wakazi wa Tal-afar wanashuhudia ushindi wenu huu mtukufu mlio upata kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Nakufikishieni dua na salamu kutoka kwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh.w), hakika muda wote anakuombeeni dua nyie pamoja na ndugu zenu wanaopigana pamoja nanyi, mpate ushindi wa haraka na kumaliza fitina hii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Nawashukuru kwa niaba ya watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu na katibu wake mkuu pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ambao wanakuombeeni dua na wanakusalimieni sana, namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akupeni ushindi na ajalie shambulio lenu kua ni shambulio litokalo katika roho ya mu-umin kwenda katika shingo la asiekua mu-umin.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awapandishe cheo kama mlivyo furahisha nyuso zetu kwa huu ushindi mkubwa mliopata, tunaendelea kumuomba atufikishe salama katika siku ambayo tutakomboa kila ncha ya aridhi ya Iraq, tunabusu mikono yenu na nyuso zenu tukufu kwa kazi kubwa mnayo fanya, amani iwe kwenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: