Atabatu Abbasiyya tukufu yashindikiza mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) walio pata shahada katika vita ya kumboa mji wa Tal-afar..

Maoni katika picha
Amani iwe kwenu enyi nafsi takatifu mliochagua kwenda kwa Mola wenu mkiwa mmeitikia wito wa aqida sahihi, Mwenyezi Mungu kakubali mwitikio wenu baada ya kumea vyema katika nafsi zenu. Amani iwe kwenu enyi nyota mng’aao, mmepokelewa na Malaika wa mbinguni kufuatia utukufu wa shahada zenu, jambo hili halipati ispakua mwenye hadhi kubwa. Kwa fahari kubwa na utukufu; kikosi cha Abbasi (a.s) kimeshindikiza mashahidi wake wanne, ambao ni:

Shahidi jemedari Hussein Dailamiy Abdu-Ali.

Shahidi jemedari Sajjaad Hussein Ali.

Shahidi jemedari Haidari Hashim Abdu.

Shahidi jemedari Tahsin Abdu-Ridha Abdul-Hussein.

Walipata shahada katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh. Walifanyiwa ziara na kuswaliwa katika haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s), kisha wakabebwa hadi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), napo ikasomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi, Imamu Ridha na Swahibu Zamaan (a.s) kwa niaba yao.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulitoa tangazo la kuomboleza mashahidi hawa watukufu ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ifuatayo ni nakala ya tangazo hilo:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mtukufu, (Wala msidhanie waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wapo hai wanapata riziki mbele ya Mola wao), Atabatu Abbasiyya tukufu kwa masikitiko makubwa inatangaza kuwashindikiza mashahidi wake watukufu kutoka katika kikosi cha Abbasi (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awadumishe peponi chini ya rehema zake, hakika yeye ni mpole na mwingi wa huruma, hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: