Haya ndiyo aliyo husia Marjaa dini mkuu kwa wakombozi wa Tal-afar..

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu hakutosheka na kutoa fatwa tukufu iliyo ihami Iraq na mashariki ya kati kwa ujumla baada ya kupata mwitikio mzuri kutoka kwa wairaq, bali ameendelea kutoa nasaha na ufafanuzi mbalimbali kwa muda wote wa miaka mitatu sasa, kwa ajili ya kuhakikisha fatwa hiyo inazaa matunda mazuri na kuepusha makossa yanayo weza kutokea hapa na pale.

Marjaa dini mkuu anatumia fursa hii kubainisha ramani ya mafanikio ya duniani na akhera, leo katoa usia kwa jeshi la Iraq na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi kuhusu vita ya kukomboa mji wa mwisho uliokuwa unashikiliwa na magaidi ya Daesh katika mkoa wa Nainawa wilaya ya Tal-afar.

Usia huo umekuja katika khutuba ya swala ya Ijumaa ya (2 Dhulhijjah 1438h) sawa na (25 Agosti 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Shekh Karbalai (d.i) miongoni mwa aliyosema ni:

  • 1- Kuchukua tahadhari dhidi ya adui Daesh pamoja na kuonekana kuvunjika moyo kwa baadhi ya vikundi vyake.
  • 2- Kusonga mbele kuzingatie mbinu makini za kivita.
  • 3- Kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu na kua na yakini ya msaada wake na nusra yake pamoja na kumuomba zaidi awape nguvu na kuwalinda.
  • 4- Kulinda uhai wa raia waliokwama ndani ya mitaa yenye vita na kuhakikisha hawapatwi na adha yeyote.
  • 5- Kuchukua tahadhari kubwa kufuatia vitimbi vya adui vya kutumia raia kama ngao yake ya kibinadamu, na kutumia kila aina ya uweledi kuwaokoa raia hao kwa muda mfupi kadri itakavyo wezekana, pamoja na kuwaandalia kambi zitakazo kua na huduma muhimu zote za kibinadamu.
  • 6- Kudumisha mawasiliano ya karibu baina ya vikosi vyote vinavyo shiriki katika vita, ambapo matunda yake ndio haya tuliyo ona, kusonga mbele kwa haraka na kufikia malengo kwa urahisi ya kukomboa mitaa kadhaa ndani ya mji wa Tal-afar kwa siku chache sana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: