Kufuatia kuwepo kwake katika mstari wa mbele huko Tal-afar: Sayyid Swafi atembelea majeruhi wa vita hiyo na asifu jitihada zinazo fanywa na madaktari..

Maoni katika picha
Kufuatia uwepo wake mstari wa mbele katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, mwakilishi wa Marjaa dini mkuu na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), ameenda kuwajulia hali wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi walio jeruhiwa katika vita hiyo na kuendelea kutibiwa katika hospitali ya Shaheed Jaasim Shibri.

Akiongozana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), pamoja na jopo la viongozi wengine wakiwa na naibu rais wa uongozi wa Hashdi Sha’abi Haji Abuu Mahdi Almuhandisi, waliwasili katika hospitali ya Shaheed Jaasim Shibri, na kupokelewa na mkuu wa Madaktari (waganga) wa Hashdi, dokta Ali Khafaaf na jopo la madaktari (waganga) wanaohudumu katika hospitali hiyo muhimu katika eneo hili.

Baada ya kutembelea wodi za hospitali hiyo na kuangalia hali za majeruhi walio lazwa hapo, Sayyid Swafi aliwaombea dua wapone haraka na warejee salama katika familia zao, pia alipewa maelezo na madaktari kuhusu huduma zinazo tolewa katika hospitali hiyo na vifaa tiba walivyo navyo, baada ya maelezo hayo; alisifu juhudi kubwa wanazo fanya madaktari za kuwatibu majeruhi na akawathibitishia kua wao ni watu muhimu sana katika vita, kwani wao ndio tumaini la afya za watu wanaojeruhiwa vitani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: