Muhimu: Kikosi cha Abbasi (a.s) chatangaza kukamilisha jukumu kililopewa katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar na chasisitiza kua wapo tayali kutekeleza jukumu lolote watakalo pewa..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) asubuhi ya Juma Mosi (3 Dhulhijjah 1438h) sawa na (26 Agosti 2017m), kimetangaza rasmi kukamilika kwa jukumu walilopewa katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar.

Nakala ya tangazo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

(Tekelezeni Ahadi hakika! Mtaulizwa kuhusu ahadi) amesema kweli Mmwenyezi Mungu mtukufu.

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake, jana tarehe (25/08/2017m), tumetimiza ahadi na kukamilisha jukumu tulilo pewa katika vita ya mkoa wa Nainawa, opreshen ya (Tunakuja ewe Tal-afar), tumekamilisha majukumu yote tuliyo pewa, na sasa hivi tupo tayali kutekeleza jukumu lolote tutakalo pewa, tutaendelea kua upanga mkali wa Abbasi dhidi ya kila muovu anayetaka kuharibu amani na utulivu wa Iraq na maeneo yake matakatifu.

Tunatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari tutakao toa maelezo kamili ya vita.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kimeshiriki katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, kikiwa na wapiganaji elfu tano, walio gawanywa katika brugedi tatu; ya mizinga, watembea kwa mikuu, na brugedi ya mikakati, katika hatua ya kwanza wamefikia malengo yao yote na wametoa kipigo kikali kwa adui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: