Kutolewa nakala mpya za kitabu cha mwongozo wa mwanafunzi juzu la ishirini na saba la Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha maarifa ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa nakala mpya za kitabu cha mwongozo wa mwanafunzi juzuu la –Dhaariyaat- ambalo ni juzu la ishirini na saba la Qur’an tukufu, hiki ni miongoni mwa vitabu vilivyopo katika selebasi ya masomu, kimeandikwa baada ya kuona mafanikio makubwa yaliyo patikana katika vitabu vya aina hii vilivyo andikwa kabla ya kitabu hiki, ambavyo ni; mwongozo wa mwalimu juzu la 30 na mwongozo wa mwanafunzi juzu la 29 na 28.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo cha maarira ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau-dini Zubaidiy, nakala hii ni sawa na nakala zilizo tangulia, zimejaa riwaya za maimamu wa Ahlulbait (a.s) zilizo hakikiwa na zinazo kubaliana na shuhuda za Qur’an tukufu, na maandishi yake ni mazuri yenye rangi murua isiyo umiza macho, inaanza kuandikwa sura au aya za Qur’an kama zilivyo kwenye msahafu, katika ukurasa kwa kwanza, kisha ukurasa unao fuata zinaandikwa maana na maelezo ya baadhi za aya pamoja na riwaya moja au mbili kutoka kwa Ahlulbait (a.s) zinazo husiana na maana za aya hizo.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya hapo tunabainisha maana kusudiwa iliyo elekezwa na Ahlulbait (a.s) pamoja na kufafanua mapokeo ya riwaya, halafu tumeandika maana za maneno katika kila ukurasa, kwani kila neno linahitaji kufahamika vizuri maana yake, maana za maneno hayo hazitakiwi kupingana na riwaya, katika vitabu vingine utakuta baadhi ya maana za maneno zinapingana na riwaya za Ahlulbait (a.s), tumejitahidi kuhakikisha maana za maneno hazipingani na riwaya tukufu, hivyo kitabu hiki kimekidhi sifa ya kua mwenendo wa vizito viwili visivyo pingana; Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu, kimefafanua kwa uwazi na ni kizuri sana kwa wanafunzi”.

Kumbuka kua kituo cha maarifa ya Qur’an, kuifasiri na kuichapisha hutoa machapisho mbalimbali kuhusu Qur’an tukufu, miongoni mwa machapisho hayo ni hili la mwongozo wa mwalimu na mwanafunzi, kitabu hiki; kimekubalika sana katika shule za kiislamu zinazo fundisha Qur’an tukufu, na kimeingizwa rasmi katika selebasi za masomo za shule hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: