Atabatu Abbasiyya tukufu yabeba gharama ya kuwapa viungo bandia majeruhi..

Maoni katika picha
Miongoni mwa huduma za kibinadamu inazo toa, Atabatu Abbasiyya tukufu imebeba jukumu la kugharamia uwekaji wa viungo bandia kwa watu kadhaa walio poteza viungo vyao, zoezi hilo linafanywa katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini yake, kwa kutumia shirika la kiholandi lililo bobea katika utengenezaji wa viungo vya binadamu tawi la Iraq.

Wale waliopoteza viungo; baada ya kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Alkafeel, jopo la wataalamu huwafunga viungo vingine vya bandia.

Mkuu wa shirika la kiholandi linalo husika na kutengeneza viungo hivyo katika tawi la Iraq, alisema kua: “Viungo hivi ni vya kisasa zaidi, vimetengenezwa kwa ustadi na ubora wa hali ya juu, kuna viungo vya kumfunga mtu ambaye mguu wake umekatikia juu ya goti na kuna vile vya kumfunga mtu ambaye mguu wake umekatikia chini ya goti”.

Akaongeza kusema kua: “Shirika la Ossur linalo tengeneza viungo hivi ni miongoni mwa mashirika makubwa duniani ya kutengeneza viungo vya binadamu, makao makuu yake yapo nchini Holandi katika mji wa Islandi, wataalamu wake wamefungua milango ya ushirikiano na hospitali ya rufaa Alkafeel, ambapo tunatarajia uhusiano huo utahusisha mambo mengi hapo baadae, shirika hilo kwa kushirikiana na hospitali ya Alkafeel siku za nyuma waliwawekea viungo bandia majeruhi sita, zoezi hilo lilipata mafanikio makubwa sana.

Akasisitiza kua: “Hakika wataalamu wa kigeni chini ya shirika la Ossur humuandaa mgonjwa na humpa mazoezi ya namna ya kutumia kiungo bandia, pamoja na kuhamisha ujuzi huo kwa wataalamu wa hospitali ya Alkafeel”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel, tembelea mtandao wa hospitali ufuatao: www.kh.iq au piga simu namba: 07602344444 au 07602329999.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: