Miongoni mwa malengo makuu ya makumbusho ya Atabatu Abbasiyya (Ni! Kulinda na kutunza vifaa kale) watalamu wanaofanya kazi katika makumbusho ya Alkafeel wamekamilisha ukarabati wa dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuliweka mahala maalumu kwa ajili ya maonyesho katika makumbusho hiyo.
Dirisha lililo fanyiwa ukarabati lilitengenezwa tangu mwaka (1182h), nalo ni miongoni mwa madirisha nadra sana, na lenye thamani kubwa, lilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu na lilikua na thamani kubwa sana katika zama hizo, nalo limepitia zama muhimu katika hatua za ujenzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ustadh Swadiq Laazim rais wa kitengo cha makumbusho amesema kua: “Tangu kuanguka kwa serikali iliyo pita mwaka (2003m), tunafanya kazi ya kukarabati dirisha la zamani la Abulfadhil Abbasi (a.s), lililo tengenezwa kwa ubora wa hali ya juu katika zama ambazo hakukua na teknolojia za kisasa, (ni zao la kazi ya mikono) hili ni miongoni mwa madirisha nadra na ya thamani kubwa, limefanyiwa matengenezo na mafundi wanaohudumu katika makumbusho yetu tukufu”.
Ustadh Amiri Ahmadi Hashim, kionozi wa idara ya ukarabati katika makumbusho ameelezea baadhi ya matengenezo waliyo fanya, akasema kua: “Tulikusanya vipande vipande vya dirisha hili vilivyo kua vimeharibika na tukaanza kuvitendeneza hadi vikarudisha muonekano wake halisi, katika matengenezo haya tuliongeza baadhi ya vitu kwa ajili ya kuweka uimara zaidi lakini tumebakisha muonekano na umbile lake la asili”.
Kumbuka kua dirisha lililopo hivi sasa katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) limetengenezwa katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu, mahsusi kwa kutengeneza madirisha ya Maimamu watakasifu na mawalii wa Mwenyezi Mungu (Ataba na Mazaru tukufu), dirisha hilo limetendenezwa katika ubora mkubwa sana, ni zuri na imara zaidi, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa hapa Iraq tena chini ya wataalamu waki-iraq miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), lina vitu vingi vinavyo lifanya kua dirisha la pekee, na kulifanya kua bora kuliko madirisha mengine yote yaliyopo katika malalo matakatifu.