Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu washiriki katika sherehe ya wanafunzi wa Barsa waliofaulu na wawataka waendelee kufaulu..

Sehemu ya sherehe
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika sherehe za wanafunzi wa vyuo, Maahadi na sekondari walio faulu katika mkoa wa Basra, kwa kuhudhuria hafla maalumu ambayo hufanywa kila mwaka ya kuwapa zawadi wanafunzi wanao faulu, hafla hiyo hufanywa kwa kushirikiana vyuo mbalimbali kikiwemo chuo kikuu cha Basra pamoja na uongozi wa malezi chini ya usimamizi wa ofisi ya mwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika mkoa wa Basra.

Ushiriki wa sherehe hii, iliyo fanyika katika chuo kikuu cha Rasulul-A’dham (s.a.w.w) katika wilaya ya Zubair, ni moja ya sehemu nyingi ambazo hushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya mpango wake wa kujenga uhusiano mwema na watu mbalimbali hususan wanafunzi na vijana.

Mwakilishi wa Marjaa dini katika mkoa wa Basra Shekh Muhammad Falak katika mawaidha yake amesema kua: “Marjaa dini wameamua kua walezi wa hafla hizi kila mwaka kwa ajili ya kujenga moyo wa kushindana kimasomo baina ya wanafunzi, na kuwapa zawadi ni jambo kubwa kwa maendeleo ya elimu katika nchi yetu ya Iraq, kwa kuzingatia kua wao ni nguzo muhimu ya ustawi wa taifa”.

Kiongozi wa Rabitu Mustafa alisema kua: “Kila mwaka Rabitu huandaa zawadi kwa wanafunzi walioshika nafasi za kwanza kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq na vituo vyake, hali kadhalika kutoka katika Maahadi na shule za upili (sekondari) wa kombi zote”. Akasema kua: “Hafla hii tunatoa zawadi kwa wanafunzi (62) kutoka katika vyuo vikuu vya Basra, na wanafunzi (61) walio shika nafasi za kwanza kutoka katika shule za upili (sekondari), pia tunawapa zawadi wakuu wa shule zilizo fanya vizuri pamoja na wakuu wa vitengo na idara zilizo fanya vizuri”.

Mwishoni mwa sherehe hii, wanafunzi wakapewa vyeti na zawadi, kamati ya maandalizi uliwapa heshima ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya ya kusimamia zoezi hilo, hivyo ugeni huo ukasimamia jambo hilo, na kuwataka wanafunzi hao waendelee kufanya vizuri katika masomo yao kwa manufaa ya taifa lao la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: