Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi wanao tibiwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, hospitali ambayo inafanya kila aina ya juhudi kutoa huduma bora za matibabu kwa watu hawa watukufu, watu waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kukomboa aridhi tukufu ya Iraq, na wakapata majeraha wakiwa katika mapambano dhidi ya magaidi ya Daesh.
Ugeni huo uliongozwa na Sayyid Adnaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamewajulia hali na kuangalia huduma za matibabu wanazo pewa, amesifu ushujaa wao na kusema kua; kutokana na damu zao takatifu wameweza kuhami aridhi tukufu ya Iraq na maeneo yake matakatifu.. kutokana na jihadi mmelinda umoja wa taifa la Iraq.. na akawaombea wapone haraka, na Mwenyezi Mungu awatunuku afya njema daima, hali kadhalika aliwafikishia salamu za watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu na dua zao kwao, na akawapa zawadi kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Pia alipongeza huduma nzuri zinazotolewa na wahudumu wa hospitali ya rufaa Alkafeel, na akawataka waendelee kutoa huduma bora zaidi kwani watu hawa tunatakiwa kuwafanyia kila aina ya uzuri kutokana na utukufu wao kwetu.
Majeruhi kwa upande wao; walionyesha shauku kubwa ya kupona haraka ili warudi katika uwanja wa vita, wakashirikiane na wenzao katika vita takatifu, wakautaka ugeni huo uwafikishie salamu na shukrani zao kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa namna wanavyo watumikia na kuwahudumia jambo ambalo limewaongezea zaidi moyo wa kuendelea na mapambano na kujitolea zaidi kwa ajili ya taifa na raia wake.
Kumbuka kua ziara hii ni miongozi mwa ziara nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu za kutembelea familia za mashahidi na majeruhi katika mikoa yote ya Iraq, kama sehemu ya kutekeleza agizo la Marjaa dini mkuu, na kuonyesha namna tunavyo thamini mihanga ya wairaq watukufu, hospitali ya rufaa Alkafeel, kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), inawapa umuhimu mkubwa majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, na imesha tibu mamia ya majeruhi hao.