Kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria: Maahadi ya Qur’an kitengo cha wanawake katika Atabatu Abbasiyya yafunga semina zake za kiangazi..

Maoni katika picha
Hafla kubwa, ndani ya mji wa Qur’an inayo tamka Ali bun Abutwalib (a.s) Najafu Ashrafu, Maahadi ya Qur’an idara ya wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya yafunga semina za Qur’an katika mwaka huu majira ya kiangazi, kwa kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i).

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha maalum kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), ambaye alipongeza ushindi wa jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi dhidi ya nguvu za ukafiri na upotofu.. na akatoa pongezi kubwa kwa kina dada kutokana na juhudi yao ya kufundisha Qur’an tukufu, na akawaomba wadumu katika kazi hii takatifu.

Hali kadhalika akatoa pongezi za dhadi kwa wanafamilia walio wapeleka bindi zao kwenda kujiunga na masomo hayo, akasisitiza umuhimu wa kutumia muda vizuri kwa kukaa katika visomo vya Qur’an tukufu, pia alisifu mafanikio ya semina hii, na akawataka washiriki waendelee kujitahidi katika masomo yao ya shule ili wapate utukufu wote wa dini na elimu.

Mwisho wa ujumbe wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, alisifu juhudi zinazo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na umuhimu wa kuendesha semina za aina hii zenye faida kubwa katika dini na madhehebu, semina zinazo fuata mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watoharifu (a.s), akasisitiza kua Qur’an tukufu ndio msingi mkuu wa malezi bora na utukufu wa kila aina.

Hafla ilipambwa na maonyesho ya Qur’an yaliyo fanywa na wahitimu wa semina, kisha dokta Swafaau Mussawiy Mkuu wa chuo cha Alkafeel katika mkoa wa Najafu akapewa zawadi kutokana na huduma alizotoa kwa wanasemina, na wahitimu wa semina hiyo nao wakapewa zawadi.

Pembezoni mwa hafla hiyo, yalifunguliwa maonyesho ya Qur’an tukufu, yaliyo husisha kazi za wanafunzi (wanasemina) ambapo kulikua na maonyesho ya hati za Qur’an pamoja na mapambo mbalimbali na kazi za mikono zilizo pamba mafanikio ya semina zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: