Uwanja wa haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wapanbwa na rangi nyeusi ishara ya kuomboleza..

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kumbukumbu ya kuawa kishahidi kwa Imamu Muhammad Baaqir (a.s) ambayo itaangukia siku ya kesho Juma Tano (7 Dhulhijjah 1438h) sawa na (30 Agosti 2017m), hali ya Atabatu Abbasiyya ni sawa na Ataba zingine na mazaru matukufu, zote zipo katika hali ya huzuni na maombolezo, wakikumbuka misukosuko aliyo ipata Imamu Baaqir (a.s) kuanzia kufariki baba yake Imamu Sajaad (a.s) hadi kufariki kwake.

Kuta za ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimepambwa kwa vitambaa vyeusi na kumewekwa mabango yaliyo andikwa riwaya mbalimbali zinazo tukumbusha tukio hilo la kuhuzunisha, na zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu, hii yote ikiwa ni ishara ya majonzi na huzuni pamoja na kumpa pole Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watoharifu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili ya maombolezo haya, kutakua na majlisi za usiku na kufuatiwa na qaswida za maombolezo kutoka kwa muimbaji mashuhuri Baasim Karbalai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: