Machozi ya waumini yabubujika katika kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu wa tano Muhammad bun Ali (a.s)..

Maoni katika picha
Kwa mbubujiko wa machozi na huzuni kubwa inayo tokana na ufuasi wa kweli, tunazipeleka rambirambi zetu kwa watu wa Kisaa na kizazi kitakasifu (a.s) hususan Hoja ya Mwenyezi Mungu katika zama hizi Imamu Mahdi Msubiriwa (a.f), na kwa Marjaa watukufu na viongozi wote wa waislamu kufuatia tukio la kuuawa kishahidi kwa imamu wetu wa tano Muhammad bun Ali Baaqir (a.s).

(Imamu –a.s- anajulikana kama..) Mtu aliye pupia elimu ya waliotangulia na wajao, aliye ipa nguvu sheria ya babu yake Mbora wa Mitume (s.a.w.w), aliye husiwa kua khalifa na Imamu baada ya baba yake Zainul-abidina (a.s), na ndiye ambaye Mtume (s.a.w.w) alimuambia Jaabir bun Abdillahi Answaariy kua: “Hakika wewe utabakia hai hadi ukutane na mwanangu Muhammad bun Ali (a.s), jina lake (sawa) na jina langu na sifa zake (sawa) na sifa zangu, atapata elimu ya dini mapema (mno), utakapo kutana nae mpe salamu zangu).

Nasaba yake ni: Muammad bun imamu Ali bun imamu Hussein bun imamu Ali bun Abutwalib (a.s), jina lake la laqabu (sifa) ni, Baaqir. Na mama yake ni Fatuma bint imamu Hassan bun Ali (a.s).

Alizaliwa mwezi mosi Rajabu mwaka wa (57h), katika mji wa Madina, aliishi (a.s) miaka hamsini na saba, mitatu aliishi na babu yake imamu Hussein (a.s) na akaishi na baba yake imamu Sajaad miaka thelathini na tano kasoro miezi miwili, muda wa uimamu wake ulikua miaka kumi na tisa na miezi miwili, umri wake (a.s) unafanana na umri wa babu yake imamu Hussein (a.s) pamoja na umri wa baba yake imamu Sajaad (a.s).

Mwanzoni mwa uhai wake alishuhudia mauaji ya Twafu (Karbala) yaliyo fanywa na Bani Umayya na vibaraka wao, katika utoto wake alipitia maisha ya mateso waliyo yapata watu wote wa nyumba ya mtume (a.s), alikua katika msafara wa mateka (wa Karbala), alishuhudia misukosuko aliyo pata baba yako kutoka kwa wafalme waovu wa zama zile takriban miaka ishirini.

Umashuhuri wa imamu (a.s), alijulikana kama: Mtu mwenye elimu kubwa, elimu yake ilionekana na kujulikana katika zama za kuenea kwa falsafa ya kiyunani na mijadala ya kielimu, pamoja na kuchomoja kwa madhehebu za kifiqhi na masomo ya ki-itikadi, mazingira hayo yalihitaji kupatikana kwa mtu mwenye elimu kubwa, atakaye weza kufundisha fikra sahihi za uislamu asili na kusahihisha mitazamo ya kifiqhi, ndipo akafungua chuo kikuu (jaamia) cha Ahlulbait na kutoa wanazuoni (wahitimu) wengi sana, watu walitoka kila sehemu wakaenda Madina kusoma elimu ya dini kwa imamu Baaqir (a.s).

Imamu Baaqir (a.s) aliuawa kishahidi kwa sumu aliyo pewa na khalifa wa kibani Umayya, inasemekana aliwekewa sumu katika tandiko la farasi na inasemekana aliwekewa katika juis (kinywaji), alipewa sumu wakati anarudi Madina kutoka Damaskas (Sham), mfalme aliye muwekea sum anaitwa Hisham bun Abdulmalik. Imamu (a.s) alikua mnene, sumu ilimuathiri mwili mzima hadi miguuni, akaugua siku tatu, ilipofika Juma Tatu mwezi saba Dhulhijjah mwaka wa (114) hijiriyya, imamu akaaga dunia. Hakika alikufa kifo cha kudhulimiwa, aliuawa shahidi kwa kupewa sumu, akazikwa katika makaburi ya Baqii ndani ya mji mtukufu wa Madina, sehemu aliyo zikwa Abbasi bun Abdulmutwalib, pia ndio sehemu aliyo zikwa baba yake Imamu Sajaad (a.s) na ammi wa baba yake, Imamu Hassan Almujtaba (a.s), vilevile ni karibu na kaburi la bibi yake Fatuma binti Asadi mama wa kiongozi wa waumini Ali bun Abuutwalib (a.s). usiku wa kufariki kwake alimuambia mwanae Imamu Swadiq (a.s): (Usiku huu nitaondoka katika hii dunia, nimemuona mzazi wangu kaniletea kinywaji kizuri na nikakichukua, akanibashiria kwenda katika nyumba ya milele na ya haki).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: