Maukibu ya Ataba mbili tukufu yahuisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Muhammad Baaqir (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na mnasaba wa kuuawa kishahidi kwa Imamu Muhammad bun Ali Baaqir (a.s), siku ya Juma Tano (7 Dhulhijjah 1438h) sawa na (30 Agosti 2017m) Maukibu ya watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ilifanya maombolezo.

Kawaida watumishi wa Ataba mbili hufanya pamoja kumbukumbu za kuzaliwa au kufariki kwa Imamu (a.s) na mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) hushirikiana nao katika viwanja hivi vitakatifu.

Msafara wa maombolezo ulianzia katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ukitanguliwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba kuelekea katika Atabatu Husseiniyya kwa kupitia katika uwanja mtukufu unaotenganisha haram mbili.

Walipo wasili katika ukumbi wa haram ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) walipokewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, kisha wakafanya majlisi ya maombolezo ya pamoja ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), wakati wakitembea kuelekea katika haram ya Imamu Hussein (a.s) walikua wanaimba qaswida za maombolezo zilizo jaza huzuni katika msafara huo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilitangaza maombolezo na kupamba haram tukufu kwa bendera nyeusi na mabango yaliyo andikwa hadithi mbalimbali kuhusu msiba huu, hali kadhalika imeandaliwa mimbari rasmi kwa ajili ya mihadhara ya kidini kuhusu matukio ya kuhuzunisha na dhulma alizo fanyiwa Imamu (a.s) pamoja na wafuasi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: