Baada ya kumaliza vita ya Tal-afar, majemedari wa kikosi cha Abbasi wapata mapokezi makubwa..

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamepata mapokezi makubwa baada ya kurudi katika mkoa wa Karbala siku ya jana Juma Tano (7 Dhulhijjah 1438h) sawa na (30 Agosti 2017m), huku wamebeba bendera za Allahu Akbaru (Mungu mkubwa), wakiwa na ushindi uliopatikana kwa mikono yao pamoja na wale walio shirikiana nao katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar uliopo katika mkoa wa Mosul kutoka mikononi mwa magaidi na matakfiri ya Daesh, watu waliofanya uharibifu katika aridhi hiyo miaka mitatu takriban, hadi Mwenyezi Mungu mtukufu kwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) na ushujaa pamoja na uzalendo wa majemedari wa kikosi cha Abbasi pamoja na wapiganaji wengine watukufu wamefanikiwa kurudisha aridhi ya mji huo chini ya umiliki wa serikali kuu, hakika wapiganaji hao wamepata mapogezi makubwa sana yaliyo ongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.i) pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na familia za wapiganaji.

Mapokezi haya ni kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza pamoja na kukumbuka mashahidi na majeruhi, ambao katika kipindi chote hiki wameonyesha ujasiri mkubwa unao tukumbusha kisha cha Karbala, kutokana na ujasiri wao wameweza kupata ushindi kwa siku chache sana ambazo hakuna aliyekua dhania hilo.

Tunatarajia kukamilika kwa ushindi wa mwisho Inshallah.

Majemedari wa kikosi cha Abbasi wamepokelewa kwa tahliil, takbiir, swala za mtume na vijinjo kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi huo, watu wa Karbala pamoja na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walijipanga mistari kuwapokea kwa shangwe kubwa huku kufurahia ushindi waliopata vijana hawa watukufu.

Wapiganaji nao walionyesha furaha kubwa kwa kurudi salama katika mji wa Karbala wakiwa na ushindi kwa kukomboa mji wa Tal-afar, na wakawashukuru watu wote waliojitokeza kuwapokea, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi wetu na awaponye haraka majeruhi watukufu.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kimeshiriki katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, kikiwa na wapiganaji elfu tano, walio gawanywa katika brugedi tatu; ya mizinga, watembea kwa mikuu, na brugedi ya mikakati, katika hatua ya kwanza walifikia malengo yao yote na walitoa kipigo kikali kwa adui.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: