Nataka kuuawa kishahidi sasa hivi!! Kisa cha mwanajihadi mzee wa miaka sabini na Sayyid Ahmad Swafi (d.i)..

Maoni katika picha
Kama mtu aliye shuhudia kazi inayo fanywa na wapiganaji katika kukomboa nchi na maeneo matakatifu.. Muwakilishi wa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swasi (d.i) akiwa katika mimbari ya swala ya Ijumaa ya leo (9 Dhulhijjah 1438h) sawa na (1 Septemba 2017m), amehadithia msimamo wa kishujaa ulio onyeshwa na mzee wa miaka sabini ambaye alitamani kua wa kwanza kupata shahada kabla ya watoto wake watano waliopo katika uwanja wa vita.

Alisema: “Alinijia mzee wa miaka sabini, akasema: Hakika nina miaka sabini, hata ukimuona ni wazi anafika umri huo, akasema: Nina watoto watano na wote wapo katika uwanja wa vita, akasema: nakuombeni kitu kimoja; mniombee nipate shahada!! Huyu mzee kwa kweli anauwelewa mkubwa sana, alisema: Niombee nipate shahada, tukamuombea: Ewe Mola mruzuku shahada baada ya umri mrefu, akasema: hapana.. hii sentesi ya mwisho usiitaje katika dua, sema: Ewe Mola mruzuku shahada sasa hivi. Tukarudia kumuombea dua: Ewe Mola mruzuku shahada baada ya umri mrefu, akakataa tena, akasema: msiniombee hivyo, yaani tusiseme –baada ya umri mrefu- tukamuambia: Ondoka tukuombee dua, akasema: sio lazima kusikia mnapo niombea dua, hakika hii ni nafasi ya pekee kwangu, ya kupata shahada nikiwa katika kutekeleza fatwa tukufu ya Marjaa dini mkuu, na umri wangu unastahiki kuwepo katika uwanja wa vita, akasisitiza sana kua lazima tuondeo sentensi ya mwisho katika dua tutakayo muombea, sentensi isemayo –baada ya umri mrefu- na badala yake tuseme: Ewe Mola mruzuku shahada hivi sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: