Swala ya Iddi katika aridhi takatifu ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na uwanja wa katikati yao..

Maoni katika picha
Baada ya makundi makubwa ya waumini kutoka ndani na nje ya Iraq ufurika katika aridhi hii takatifu na kufanya ibada maalumu za usiku wa Arafa na mchana wake, wamehitimisha kwa kuswali Iddi na kuliombea taifa amani na raia wake pamoja na kuliombea ushindi jeshi la serikali pamoja na Hashdi Sha’abi.

Swala zimeendeshwa katika kumbi zote mbili tukufu, ukumbi wa haram ya Imamu Hussein na ule wa haram ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja uwanja wa katikati ya haram mbili napo palifurika waumini na swala ya sehemu hiyo ikaongozwa na Sayyid Ahmadi Swafi.

Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ulishuhudia swala ya Iddi zaidi ya mara moja kutoka na wingi wa watu walio endelea kumiminika kwa ajili ya swala hiyo, hali kadhalika katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), zilijipanga kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na vyombo vya ulinzi na usalama viliimarisha ulinzi ili kuhakikisha mazuwaru watukufu wanafanya ibada zao kwa amani na usalama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: