Kitengo cha misaada chini ya ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) wagawa chakula cha Iddi kwa wakimbizi waliopo Tikriti..

Maoni katika picha
Kufuatia sikukuu ya Iddul-Adhha na kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kusaidia familia za wakimbizi na kusimama pamoja nao katika shida na raha, kamati ya misaada chini ya ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) wamegawa chakula kilicho tolewa na taasisi ya Ain kwa wakimbizi waliopo Tikriti makao makuu ya mkoa wa Swalahu-Dini.

Sayyid Shaheed Mussawiy ambaye ndio rais wa kamati hiyo amesema kua: “Ugawaji huu wa nafaka za chakula, umefanyika baada kufanya uchunguzi na kubaini familia zenye hali mbaya zaidi, tumegawa kiasi cha vikapu 2500 vyenye aina tofauti za nafaka, chakula hicho tumezigawia familia zinazo ishi katika majengo ya serikali yaliyo hamwa na wale waliopo katika maeneo ya stendi wanaoishi katika mazingira magumu”.

Akasema kua: “Hakika watu hawa wamefurahi sana, wakasifu namna Marjaa dini mkuu anavyo wakumbuka na kuwajali na hii sio mara ya kwanza wao kupewa misaada, mmoja waao alisema kua: Kila tunapo kua na hali mbaya zaidi nyie hua mnatukumbuka na kuja kutupa misaada, mwingine akasema: Hii ni mara ya nne nakuoneni mnakuja kugawa misaada katika mji wa Tikriti, tunatoa shukrani za dhati kwenu kutoka ndani ya nyoyo zetu”.

Kumbuka kua misafara ya kutoa misaada inaendelea kama ilivyo pangwa katika miji iliyo kombolewa na katika hema za wakimbizi, kwa ajili ya kuwapunguzia machungu na kuwafanya wafahamu kua Marjaa dini mkuu ndio kimbilio sahihi la wairaq wote bila kujali makabila wala tabaka zao, na kuondoa picha mbaya inayo sambazwa na maadui, fahamu kua; familia hizi zinaishi katika mazingira magumu sana hususan kipindi hiki cha joto kali, kwani wanaishi katika majengo na maeneo ambayo sio rasmi kwa kuishi mwanadamu, idadi ya wakimbizi inaongezeka kila siku, bado zinahitajika juhudi kubwa za kuwasaidia watu hawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: