Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa Alkafeel kuhusu makumbusho yakamilisha ukaguzi wa mada zitakazo shiriki katika kongamano hilo, na yasisitiza kua kukomano litakua zuri..

Sihemu ya kikao
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa Alkafeel, litakalo endeshwa na makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu tarehe saba mwezi huu, wamesema kua awamu hii itakua nzuri zaidi kushinda awamu wa kwanza, kutokana na uboreshwaji wa kongamano hili na aina ya washiriki wake kutoka ndani na nje ya Iraq, tunatarajia kongamano hili litakua na matokea chanya katika semina zijazo na litasaidia kuboresha sekta ya makumbusho.

Taarifa ya kamati inasema kua: “Idadi ya mada zilizo wasilishwa katika kamati hiyo zilikua (63) kutoka ndani na nje ya Iraq, mada zote zilikidhi viwango vya kiuandishi, lakini mada zilizo pasishwa na zitakazo shiriki katika kongamano zitakua (20) na zitakazo wasilishwa katika kongamano zitakua mada (16) zitakazo gawanywa katika sehemu tatu ndani ya siku mbili za kongamano hilo, chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho ni mazingira na uchumi)”.

Wakabainisha kua: “Kutakua na washiriki kutoka katika nchi za kiarabu na zisizokua za kiarabu, (Misri, Ujerumani, Japani na Iran) pamoja na ushiriki mkubwa wa wairaq kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq na wadau mbalimbali wa makumbusho”.

Kumbuka kua kongamano hili ni sehemu ya program inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujuana na kubadilishana uzoefu baina ya makumbusho tofauti, na washiriki wa kongamano hili ni wadau na wataalamu wa makumbusho kutoka ndani na nje ya Iraq, kongamano linalenga mambo yafuatayo:

Kwanza: Kulinda urithi wa kimazingira na kitamaduni.

Pili: Kusaidia taasisi za dini kuanzisha makumbusho na kuendeleza kazi za makumbusho.

Tatu: Kufungua milango ya kusaidiana baina ya makumbusho za kitaifa na kimataifa na kuziendeleza.

Nne: Kuinua hadhi za makumbusho katika sekta ya habari na uchumi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: