Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) amesisitiza umihimu wa vyombo mbalimbali kuwajali mayatima hususan katika sekta ya malezi, ili kuwajengea mustaqbali mwema wenye mafanikio na kuondoa hali ya unyonge waliyo nayo, usionekane uyatima kua sababu ya kutopata maisha mazuri.
Aliyasema hayo alipo kutana na mayatima wanao lelewa na taasisi ya Imamu Sajaad (a.s) katika mkoa wa Karbala baada ya kumaliza kula katika mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) leo Juma pili (11 Dhulhijjah 1438h) sawa na (3 Septemba 2017m).
Aliongeza kusema kua: “Hakika watu hawa wana umuhimu mkubwa sana katika jamii, ukilinganisha na mazingira ya vita na matatizo mbalimbali ambayo taifa linapitia kwa sasa, ni wazi kua tunatakiwa kuwajali na kuwapa kila aina ya msaada pamoja na kushirikiana na taasisi zinazo walea”.
Naye Mheshimiwa Sayyid Adnaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini alitoa muhadhara, miongoni mwa aliyo sema ni: “Mnafahamu kua ndoa huleta jukumu la malezi kwa baba na mama, kuna baadhi ya majukumu hua rasmi kwa ajili ya mama, ukizingatia kua mama yupo karibu sana na mtoto kushinda mtu yeyote, lakini katika hali ya kawaida tunaweza kusema jukumu la malezi nusu ni la baba na nusu la mama, anapo kosekana baba jukumu lote humuangukia mama, mama anamchango wa wazi katika malezi ya mtoto, lakini jukumu litakua kubwa kwake”. Kisha Sayyid Adnaan akazungumzia haki za yatima, na ulazima wa kutunza mali zake na kuto zitumia, akafafanua kama ilivyo andikwa katika Qur’an tukufu.
Sayyid Faadhil Hussein rais wa taasisi ya Imamu Sajjaad (a.s) aliumbia mtandao wa Alkafeel kua: “Tuna zaidi ya familia (450) za mayatima zinazo hudumiwa na taasisi, tunawapa hela mayatima kila mwezi na aina mbalimbali za nafaka za vyakula, hatuja tosheka na hilo, bali hua tunawapa mawaidha na masomo mbalimbali, hakika wao ni miti ya matunda ambayo yataiva hivi karibuni na yatasaidia katika kujenga jamii njema yenye maadili, mayatima wa taasisi hiyo wanakawaida ya kutembelea Atabatu Abbasiyya kila mwaka na kukutana na viongozi wa Ataba tukufu, katika siku ya pili ya Iddul-Adhha tukufu wametembelea Ataba na wamepata chakula pamoja na kupewa zawadi mbalimbali, haya yalifanyika baada ya kukamilisha ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hii sio mara yao ya kwanza, huja na hukirimiwa mara nyingi”.
Mayatima na familia zao walionyesha furaha kubwa sana kutokana na ukarimu walio fanyiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku hii tukufu ya Iddi pili.
Kumbuka kua program hii ni miongoni mwa utaratibu ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusaidia mayatima na kuwaandaa kijamii, ili wasijihisi unyonge kutokana na uyatima wao, kama ilivyo kwa baadhi ya mayatima.