Shirika la Bora la teknolojia ya kilimo cha kisasa limetengeneza kirutubisho kinacho boresha ukuaji wa wanyama kwa kiasi kisicho cha kawaida..

Maoni katika picha
Kama ada yake (Shirika la Bora la teknolojia ya kilimo cha kisasa..) chini ya kitengo cha uchumi katika Atabatu Abbasiyya tukufu linasonga mbele katika kukuza uwezo wake kwenye sekta ya ustawi wa mimea na wanyama, mara hii wametoa kirutubisho kipya kiitwacho (Aschomax) kimeonyesha mafanikio makubwa katika jaribio lake, kirutubisho hicho kimetengenezwa na raia halisi wa Iraq, kwa mara ya kwanza kimeonyesha mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku, kinatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa taifa.

Kirutubisho hicho, kwa mujibu wa mkuu wa shirika la Bora tajwa hapo juu, Ustadh Maitham Bahadeli amesema kua: “Ni mlo kamili, au nyongeza ya chakula; kinafanya kazi ya kunenepesha mnyama na kinampa afya njema na kumfanya akuwe haraka”

Akaongeza kusema kua: “Kirutubisho hiki ni rasmi kwa ajili ya wanyama wa aina za ndege, kitaboreshwa zaidi ili kiweze kuhusisha aina zingine za wanyama, nacho huchanganywa katika chakula cha wanyama kwa ajili ya kusaidia makuzi na kuboresha afya ya nyama”.

Akafafanua kua: “Tumefanya jaribio katika mkoa wa Waasit, banda moja tuliweka vifaranga (6500) na banda lingine tukaweka vifaranga idadi hiyo hiyo, vyenye sifa sawa na vya kwanza, banda ambalo chakula kilichanganywa na kirutubisho cha (Aschomax) baada ya siku (32) kuku mmoja walikua na uzito wa gram (1850) na kiasi cha kuku waliopata maradhi walikua (85), huku banda la pili ambalo chakula chake hakikuchanganywa na kirutubisho hicho, baada ya siku (35) kuku mmoja alikua na uzito wa gram (1700), na kuku walio pata maradhi walikua (580), hivyo! Matokeo ya utafiti yako wazi kama yanavyo onekana hapo juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: