Majemedari wa kikosi cha Abbasi wazuia shambulio la magaidi katika mji wa Sayyid Muhammad (a.s)..

Maoni katika picha
Majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamefanikiwa kuzuia shambulio la magaidi katika mji wa Sab’u Dujail Sayyid Muhammad (a.s) jioni ya jana.

Kikosi cha wapiganaji wa Abbasi kilichopo katika mji wa Balad pamoja na wanajeshi wa serikali walifanikiwa kuwazingira magaidi watano waliotaka kujiribua katika haram tukufu ya Sayyid Muhammad (a.s), wawili walilazimishwa kujiripua mbali na sehemu za watu na hawakuleta madhara yeyote, huku magaidi watatu wakifanikiwa kukimbia na kutokomea kusiko julikana, wapiganaji wetu watukufu wanafanya msako mkubwa katika mashamba yeto yanayo zunguka eneo hili.

Kwa upande mwingine, wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) waliopo katika mji wa Mosul kitongoji cha Badush wamefanikiwa kuua magaidi wawili waliotaka kujiripua katikati ya raia.

Kikosi cha Abbasi (a.s) kumethibitisha ahadi yake kwa wananchi kua; wao wako macho, hawatalala wala kusinzia, wamesimama imara kulinda usalama wao, matukio haya yametoa matumaini makubwa kwa wananchi kua amani ya raia wa Iraq inalindwa na watu wenye uwezo wa kuimarisha usalama wakati wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: