Maandalizi ya Iddi kubwa: Kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) lapambwa kwa maua..

Maoni katika picha
Kufuatia maandalizi matukufu ya Iddi kubwa –Iddul-Ghadir tukufu- dirisha la kaburi takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa kwa maua mazuri, kwa namna ambayo linaingiza furaha katika nyoyo za watu wanaokuja kufanya ziara kufuatia mnasaba huu mtukufu.

Aina hii ya maua yaliyo wekwa, ni miongoni mwa maua mazuri na yenye thamani kubwa, hutengenezwa kwa umaridadi mkubwa kwa ajili ya kuwekwa katika dirisha za makaburi, pia kuna maua mengine yamewekwa katika milango ya kuingia haram, maua haya yamegharamiwa na kitengo cha ulezi wa haram wakisaidiwa na baadhi ya wahisani chini ya uratibu wa kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi zote za mapambo zimefanywa na kitengo cha ulezi wa haram, hakika upambaji unahitaji uangalifu na umakini mkubwa katika kupangilia rangi hadi muonekano wake uendane na mazingira halisi unao kubaliana na mazingira haya matukufu.

Iddul-Ghadir huzingatiwa kua sikukuu kubwa kwa waislamu ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s), katika siku hii (18 Dhulhijjah) Mtume (s.a.w.w) alitoa hutuba ndefu, katika hutuba hiyo alimtangaza imamu Ali (a.s) kua ni khalifa, wasii na kiongozi wa waislamu baada yake, hutuba hiyo aliitoa katika hijjatu widaai (hijja yake ya mwisho) wakati mahujaji wanarudi kutoka hijja, aliwakusanya katika sehemu inayo itwa (Ghadir Khum) mwaka wa kumi (10) hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: