Zijue ibada za siku ya Ghadiir..

Maoni katika picha
Siku ya Iddul-Ghadiir ambayo ni sikukuu kubwa pia ni sikukuu ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), hakika hii ni sikukuu kubwa zaidi, mitume wote walisherehekea sikukuu hii, huko mbinguni inaitwa siku ya ahadi iliyo ahidiwa na hapa duniani inaitwa siku ya kuchukua ahadi na kushuhudiwa na umati.

Siku hii lazima ipewe heshima yake, zimesuniwa ibada mbalimbali katika siku hii tukufu, miongoni mwa ibada hizo ni:

Kwanza: Kufunga; nayo ni kafara ya miaka sitini, pia imepokewa kua funga yake unaandikiwa dhawabu za funga ya milele, na unaandikiwa thawabu za hijja na umra mia moja.

Pili: Kuonga.

Tatu: Kumzuru kiongozi wa waumini (a.s).

Nne: Kusomo dua ya kujilinda (ta’awwadh) iliyo pokewa na Sayyid katika kitabu cha Iqbaal kutoka kwa Mtume (s.a.w.w).

Tano: Kuswali rakaa mbili, kisha unasujudu na kumshukuru Alla mara mia moja, halafu ikitoka katika sajda unasema: (Allahumma inniy as-aluka bi-anna lakalhamdu wahdaka laa sharika laka..) hadi mwisho wa dua, dua hii ipo katika kitabu cha Mafaatihul Janaan).

Kisha usujudu mara ya pili na useme katika sajda, (Alhamdulilaahi, mara 100 na Shukran lilaahi mara 100). Imepokewa katika riwaya kwamba; atakaye fanya hivyo atakua sawa na mtu aliye hudhuria na kumpongeza Mtume (s.a.w.w) katika tukio (la kumtawaza Imamu Ali –a.s-), inapendekezwa zaidi uswali karibu na kugeuka jua, ambao ndio muda alio tangazwa Ali (a.s) kua Imamu wa watu wote. Katika rakaa ya kwanza baada ya Alhamdu usome surat Alqadr na katika rakaa ya pili baala ya Alhamdu usome surat Tauhiid.

Sita: Uoge na kuswali rakaa mbili, katika kila rakaa baada ya Alhamdu usome surat Tauhiid mara 10 na Ayatul-Kursiyyu mara 10 na surat Alqadr mara 10.

Saba: Usome dua Nudba.

Nane: Usome dua hii ambayo imepokewa na Sayyid Ibun Twaus kutoka kwa Shekh Mufiid, isemayo: (Allahumma inniy as-aluka bihaqi Muhammad Nabiyyika, wa Aliyu waliyuka…) hadi mwisho wa dua, dua hii ipo katika kitabu cha Mafaatihu Janaan.

Tisa: Umpongeze kila utakae kutana naye miongoni mwa waumini.

Kumi: Useme mara 100: (Alhamdulilaahi Aladhii ja’ala kamala diinihi wa tamaami ni’imatihi biwilayat Amirilmu-uminina Aliyu bun Abiitwalib alaihi salaam).

Miongoni mwa a’amaal (ibada) za siku hii pia ni kuvaa nguo nzuri, kujipamba, kupaka mafuta uzuri, kuonyesha furaha, kuwafurahisha wafuasi wa Amirulmu-uminina (a.s), kusamehe aliye kukosea, kusaidia watu, kuunga undugu, kutembelea wana familia, kulisha chakula, kufuturisha walio funga, kupeana mikono na waumini, kutembeleana, kuonyesha tabasamu, kupeana zawadi, kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema kubwa aliyo tupa, neema ya wilaya, kumswalia Mtume (s.a.w.w) kwa wingi. Ibada yeyote utakayo fanya katika siku hii au sadaka utakayo toa, shilingi moja unalipwa thawabu sawa na mtu aliye toa shilingi laki moja katika siku zingine, na ukilisha chakula unaandikiwa thawabu sawa na mtu aliye walisha mitume wote na walio wasadikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: