Maana ya siku ya Ghadiir

Maoni katika picha
Sababu za kuitwa siku ya Ghadiir:

Siku hii imeitwa kwa jina hilo kwa sababu Mtume (s.a.w.w) kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, wakati anatoka hijja akiwa na maelfu ya maswahaba walisimama katika sehemu iliyopo baina ya Maka na Madina inayoitwa Ghadiir Khum, kwa hiyo siku imepewa jina la sehemu.

Siku ya Ghadiir ndio kitu gani?

Siku hii; Ni siku ya kumi na nane ya mwezi wa Dhulhijjah mwaka wa kumi hijiriyya. Nayo ni siku ambayo Mtume (s.a.w.w) kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Ali bun Abutwalib (a.s) kua khalifa, wasii na Imamu baada yake. Nayo ni siku tukufu sana, hadithi nyingi zimeelezea utukufu wa siku hii, katika riwaya iliyo pokewa na Imamu Ali bun Mussa Ridha (a.s) kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake anasema: “Hakika siku ya Ghadiir ni mashuhuri zaidi mbinguni kushinda duniani”.

Na kutoka kwa Imamu Jafari bun Muhammad Swaadiq (a.s) anasema: “Mbinguni inaitwa siku ya ahadi iliyo ahidiwa na duniani inaitwa siku ya kuchukua ahadi na kushuhudiwa na umma”.

Kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) anasema: “Wallahi lau watu wangejua utukufu wa siku hii, wangepewa mikono na malaika mara kumi kila siku”.

Hili ni tukio la pili kwa ukubwa katika uislamu, baada ya tukio la kupewa utume na kushushwa kwa Qur’an tukufu.

Iddul-Ghadiir:

Siku ya Ghadiir; ni siku ya sikukuu bali ndio sikukuu kubwa na tukufu zaidi, Mwenyezi Mungu mtukufu hajawahi kutuma mtume yeyote ispokua alisherehekea siku hii, kwa sababu ni siku ya kukamilisha dini na kutimiza neema. Imepokewa kutoka kwa Imamu Jafari bun Muhammad Swaadiq kutoka kwa baba yake kutoka kwa baba zake (a.s) anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema: “Siku ya Ghadiir Khum ndio sikukuu bora zaidi katika umati wangu, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu mtukufu aliniamrisha nimtangaze ndugu yangu Ali bun Abutwalib (a.s) kua ndiye bendera (kiongozi) wa umati wangu, wataongoka kupitia yeye baada yangu, na ndio siku ambayo Mwenyezi Mungu amekamilisha dini, na akakamilisha neema yake kwa umma wangu, na akaridhia dini ya uislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: