Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla iliyo pambwa na qaswida murua katika Iddul-Ghadiir..

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyo jaa furaha kufuatia sikukuu kubwa ya Mwenyezi Mungu Iddul-Ghadiir, Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia kitengo cha utunzaji wa haram tukufu, imefanya hafla kwa ya kuhuisha manasaba huu wenye nafasi kubwa sana katika nyoyo za waumini wanaofuata mwenendo wa Mtume mtukufu na watu wa nyumabani kwake watoharifu (a.s).

Hafla imefanywa jioni ya jana Juma Pili (18 Dhulhijjah 1438h) sawa na (10 Septemba 2017m) katika ukumbi wa haram ya Abulfadhi Abbasi (a.s), ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur’an tukufu, kisha muimbaji mashuhuri wa qaswida bwana Mula Thaamir Al-aaridhi, akaanza kuimba Qaswida zinazo onyesha mapenzi kwa Ahlulbait (a.s).

Baada yake akapanda katika mimbari mwimbaji mwingine bwana Mula Hussein Al-akili, akaendelea kuimba kama alivyo fanya mtangulizi wake, hakika Qaswida hizo zilifasiri hisia za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) walio hudhuria katika hafla hiyo, kutokana na uzuri wa sauti na ujumbe wa Qaswida zao ziliwafikisha wahudhuriaji katika kilele cha furaha.

Kisha akaingia mzungumzaji mashuhuri Muhammad A’ajibi, aliye hutubia kwa njia ya mashairi ya kumsifu na kuonyesha mapenzi kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abutwalib (a.s), na mwisho ikafungwa hafla kwa Qaswida iliyo somwa na Hussein Mula Alaa Albayati.

Kumbuka kua kitengo cha utunzaji wa haram tukufu, kila mwaka hua kinafanya hafla hii, ya kusherehekea kutangazwa kwa imamu Ali bun Abutwalib (a.s) kua khalifa wa waislamu na wasii wa Mtume (s.a.w.w), hafla ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kundi kubwa la watu waliokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: