Baada ya matukio ya hivi karibuni yaliyo shuhudiwa katika wilaya ya Balad, majaribio kadhaa ya kihalifu yaliyo taka kufanywa na magaidi ya Daesh na kudhibitiwa na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) waliopo katika wilaya ya Balad na mji wa Dujail, pamoja na vikosi vya Samara wakishirikiana na jeshi shujaa la Iraq.
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimeongeza wapiganaji wake katika miji hiyo ya Balad na Dujail.
Kamanda wa kikosi amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha usalama wa raia na njia kuu ya (Bagdad/ Samara), hali kadhalika kulinda kila sehemu iliyo kombolewa isishambuliwe tena na magaidi wa Daesh wanao endelea na mashambulizi ya kujilipua hapa na pale baada ya kuukosa mkoa wa Nainawa.
Kufuatia ziara ya kikazi aliyo fanya kamanda wa vikosi vya Samara vya jeshi la serikali katika maeneo yanayo lindwa na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), aliwasifu wapiganaji hao kwa ushujaa na ujasiri mkubwa walio nao pamoja na mawasiliano mazuri na vikosi vya serikali.
Kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na jeshi la serikali pamoja na kikosi cha anga walifanya msako mkubwa, wa kuwasaka magaidi ya Daesh katika mashamba yote yanayo zunguka mji wa Balad.
Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kina wapiganaji katika mji wa Balad na Dujail ambao jukumu lao kubwa ni kuhakikisha usalama wa barabara na kulinda malalo ya Sayyid Muhammad (a.s) pamoja na majukumu yeyote watakayo pewa na viongozi wa juu wa kikosi cha ushirika cha Balad na Dujail.