Kufuatia furaha za kutawazwa Qur’an yenye kutamka Ali bun Abutwalib (a.s) kua waliy na khalifa wa waislamu, kituo cha miradi ya Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya hafla ya Qur’an ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), jioni ya Juma Tatu ya (19 Dhulhijjah 1438 h) sawa na (11 Septemba 2017 m).
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Faisal Matwar, na ilikua na ushiriki mkubwa wa wasomaji wa Qur’an wa Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa walioshiriki usomaji wa Qur’an katika hafla hiyo ni; Faisal Matwar, Leeth Abidiy, Muhammad Ridha Zubaidiy na Ali Saaidiy.
Hafla ilifungwa kwa sauti ya Ali Saaidiy, baada ya kumaliza kisomo cha Qur’an tukufu ikasomwa dua ya Imamu Mahdi Almuntazil (a.f) na kuiombea Iraq ipate usalama na amani.
Hafla hii imepata mahudhurio makubwa kutoka kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa hakika walifarijika sana, kwa kusikiliza aya tukufu za Qur’an huku wakitarajia thawabu, baraka na rehema za Mwenyezi Mungu mtukufu.