Tafiti (50) kutoka ndani na nje ya Iraq zitawasilishwa katika kongamano la kimataifa Al-ameed awamu ya nne..

Maoni katika picha
Kamati ya elimu ya kongamano la kimataifa la Ameed awamu ya nne imetangaza kua tafiti (50) kutoka ndani na nje ya Iraq zitawasilishwa katika kongamano litakalo anza baada ya kesho Alkhamisi (22 Dhulhijjah 1438h) sawa na (14 Septemba 2017m) litakalo dumu siku mbili, likiwa na kauli mbiu isemayo: (Tunakutana chini ya usimamizi wa Ameed ili tujuane) na anuani nyingine isemayo: (Amani na utamaduni, uwelewa na utendaji).

Kamati imesema kua: “Tumesha pokea tafiti (70) zote ziliwasilishwa katika kamati ya masomo ya kibinadamu kwa watalamu na wahariri wa jarida la Ameed, tafiti hizo zinakidhi vigezo vya kielimu na taratibu za kiuandishi”.

Muongeaji rasmi wa kongamano hili dokta Ahmadi Swabeeh Ka’abiy amesema kua: “Nchi zitakazo shiriki zimefika (8), ambazo ni: (Uingereza, Kanada, Italia, India, Iran, Oman, Aljeria, Lebanon), pamoja na vyuo vikuu vya: (Bagdad, Karbala, Kufa, Qadisiyya, Basra, Mustanswariyya, Misaan na Baabil).

Akasisitiza kua: “Maudhui kuu ya kongamano hili ni (Amani na utamaduni), tunataka kunufaika na kalamu za wasomi katika jambo hili, hakika faida ya kua na jamii yenye maelewano na amani ni ya kila mtu”.

Mada za wazungumzaji zitahusu mambo yafuatayo:

Jambo la kwanza: Amani na utamadudi (Uwelewa na utekelezaji).

Jambo la pili: Utambulisho na amani na utamaduni.

Jambo la tatu: Jihadi na amani na utamaduni.

Jambo la nne: Elimu na amani na utamaduni.

Jambo la tano: Utandawazi na amani na utamaduni.

Jambo la sita: Malezi na amani na utamaduni.

Jambo la saba: Historia na amani na utamaduni.

Jambo la nane: Ubunifu na amani na utamaduni.

Kumbuka kua kongamano la kimataifa Ameed lilipata mafanikio makubwa katika awamu zake za nyuma, hilo limethibitishwa na kila aliye hudhuria kongamano hizo, waliweza kutengeneza njia mpya ya uwasilishaji wa tafiti za kisekula, na kuhakikisha tafiti hizo zinafanyiwa kazi na matunda yake kuonekana katika jamii, hali kadhalika wasimamizi wa kongamano hujitahidi kutekeleza maazimio yanayo fikiwa, hata hili kongamano la kimataifa la Ameed ni sehemu ya moja ya maazimio yaliyo fikiwa katika vikao vya mwanzo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: