Kutolewa nakala ya kwanza ya jarida la Taslim na kituo cha kimataifa cha Ameed lilbuhuthi wa dirasaat..

Maoni katika picha
Tafiti kumi na nne tofauti kutoka kwa watafiti wa kisekula, hivi karibuni kituo cha kimataifa Al-ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mara ya kwanza wametoa nakala za jarida la Taslim, jarida hilo limejikita katika fani za lugha.

Jarida la Taslim limeandikwa tafiti mbalimbali katika sekta ya lugha ya kiarabu ambazo zilikua hazijaandikwa hapo awali, na limefuata kanuni za kitaalamu katika uandishi wa tafiti, litapatikana katika lugha ya kiarabu na kiingereza.

Kitengo cha elimu katika kituo cha kimataifa cha Ameed duwaliyu lilbuhuthi wa dirasaat kimelifanya jarida hili kua moja ya hazina ilizo asisi za utunzaji wa elimu, kutokana na sera ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kutunza elimu na kuifanyia kazi ili kuhakikisha inaleta manufaa katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: