Kituo cha ukarabati wa nakala kale katika Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya semina kuhusu namna ya kutengeneza vitabu..

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa imamu Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Juma Tano ya (21 Dhulhijjah 1438h) sawa na (13 Septemba 2017m) imefanyika nadwa kuhusu mbinu za kutengeneza vitabu vya kiislamu, mtoa mada alikua ni dokta Rod Karry kutoka Ujerumani.

Nadwa ilikua na uwakilishi wa nchi za kiarabu na wenyeji, katika nadwa hii imeelezewa namna ya kutengeneza vitabu vya kiislamu, hasa vitabu vya zamani vilivyo andikwa karne ya kumi na tano, dokta Karry amefurahishwa na maendeleo mazuri ya Atabatu Abbasiyya katika sekta ya uchapishaji wa vitabu vya kiislamu, katika hotuba yake ameelezea namna ya kutengeneza kitabu baada ya kukifanyia ukarabati.

Ustadh Swadiq Laazim aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kufanikisha kongamano la pili la Alkafeel tulitoa mwaliko kwa dokta Karry muhadhiri wa chuo kikuu cha Balin, alipo kuja kutembelea makumbusho ya Alkafeel, na tukabaini zana zinazo hitajika katika utendaji wa kukarabati nakala kale, baada ya hapo alitoa muhadhara kwa watumishi wa makumbusho ulio husu namna na kukarabati nakala kale, hakika hiyo fani inahitaji umakini mkubwa”.

Akaongeza kusema kua: “Nadwa ilihusu namna ya kutengeneza nakala kale za kiarabu, na namna ya kupangilia kitabu kabla ya kukitengeneza ambao ndio utaratibu unaofatwa duniani”.

Kumbuka kua nadwa hii ilipata uwakilishi wa nchi za kiarabu, ulio ongozwa na dokta Saidi Abdulhamiid, mkuu wa kituo cha ukarabati wa vitabu katika jiji la Kairo, na kituo cha urekebishaji wa nakala kale cha Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na kile cha Atabatu Abbasiyya, pia walitembelea makumbusho na kuangalia vifaa vinavyo tumika katika kutengeneza vitabu vilivyo haribika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: