Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Umma wetu unakabiliwa na tishio la amani kifikra na kitamaduni, tishio hili ni hatari kubwa sawa na hatari zingine zilizopo katika umma..

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) amesisitiza kua: “Hakika umma wetu unakabiliwa na tishio la uvunjifu wa amani kifikra na kitamaduni, tishio hili ni hatari kubwa sawa na hatari zingine zilizopo katika umma, natoa wito kwa kila mtu mwenye mapenzi na umma huu atumie fursa ya kongamano la kimataifa la Ameed awamu ya nne kuangalia namna ya kupambana na tishio hili”.

Aliyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye ufunguzi wa kongamano la kimataifa la Ameed awamu ya nne lililoanza asubuhi ya leo Alkhamisi (22 Dhulhijjah 1438h) sawa na (14 Septemba 2017m) na litadumu siku mbili, chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunakutana katika kongamano la Ameed tujuane) na anuani isemayo: (Amani na utamaduni, uwelewa na utekelezaji).

Akaongeza kusema kua: “Kwa mara nyingine tunakutana katika kongamano la kimataifa la Ameed awamu ya nne, kongamano linalo tuleta pamoja na maprofesa na watafiti wanao kuja kutueleza mambo muhimu sana kifikra na kitamaduni, ambayo ni mambo ya amani na utamaduni”.

Ashiqar akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (a.i) imetoa baraka zote kwa kongamano hili, tunatarajia kunufaika na elimu ya wasomi wa sekula watuletee ufumbuzi wa changamoto zilizopo katika umma”.

Akafafanua kua: “Atabatu Abbasiyya imefungua milango ya ushirikiano na wasomi wa aina zote wa ndani na nje ya Iraq, shabaha yetu kubwa ni kuhakikisha wanachuoni wanachukua nafasi yao katika kuelekeza umma fikra sahihi, na wawe na mchango mkubwa katika kila zuri linalo hitajiwa na jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: