Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waweka mapambo ya kuashiria huzuni za Ashura katika malalo ya bibi Zainab (a.s)..

Maoni katika picha
Muendelezo wa kazi inayofanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ya ukarabati wa malalo ya jabali wa subira bibi Zainab (a.s), leo wanaendeleza kazi yao kwa kuzipamba kuta tukufu za malalo hayo kwa mapambo meusi yanayo ashiria huzuni, kwa ajili ya kujiandaa na ujio wa mwezi mtukufu wa Muharam, pamoja na kuendelea kufanyia ukarabati baadhi ya maeneo ya haram hiyo takatifu.

Rais wa kitengo cha ulezi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambaye ndiye mkuu wa msafara huo na msimamizi wa kazi zinazo fanyika huko amesema kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ugeni wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao ni kitengo cha utunzaji wa haram tukufu na kitengo cha habari na utamaduni, wamefanya kazi ya kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni katika malalo ya Aqilah bibi Zainab (a.s) huko Sirya Damaska, kwa ajili ya kuiandaa haram tukufu na huzuni za mwezi mtukufu wa Muharam”.

Akaongeza kusema kua: “Vitambaa vilivyo tumika vimeshonwa na kitengo cha ushonaji cha Atabatu Abbasiyya tukufu na vimedariziwa ujumbe maalumu kuhusu tukio la Muharam”.

Akasema: “Hali kadhalika ukarabati huo ulihusisha sistim ya sauti iliyo fungwa kwa gharama za Atabatu Abbasiyya tukufu, na kubadilisha taa zilizo kuwepo na kuwekwa taa zinazo endana na kumbukumbu ya Ashura na mwezi mtukufu wa Muharam, pia maeneo yote ya haram yamefanyiwa usafi pamoja na dirisha takatifu la malalo, hadi kubba yano imefanyiwa matengenezo na kuandaa vifaa maalumu vya kusafishia malalo hii tukufu”.

Kumbuka kua msafara huu umechukua siku kadhaa, na wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha sehemu hii takatifu inakua na muonekano mzuri zaidi katika kipindi hiki ambacho tunajiandaa na msimu wa huzuni pamoja na kuwapokea watu watakao kuja kufanya taazia, hakika watumishi wanaofanya kazi hii wameruhusiwa na uongozi wa juu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na wamefurahi kupata nafasi hii, hakika wamepata utukufu mara mbili, utukufu wa kumtumikia Abulfadhi Abbasi (a.s) na dada yake Aqilah bibi Bainab (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: