Filamu ya (Sayyidul-maau) imeshinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya filamu yaliyo fanyika kwenye kongamano la kimataifa la Alghadiir, lililofanyika katika mkoa mtukufu wa Najafu, chini ya usimamizi wa luninga ya Al-Ghadiir, likiwa na kauli mbiu isemayo (Vyombo vya habari na ujumbe wa muqawama na ushindi) ambayo ni katika kazi zilizo fanywa na studio ya Aljuud chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kwa mujibu wa Ustadh Ahmad Mamitha kiongozi wa studio hiyo alisema kua: “Filamu ya Sayyidul-maau, inaonyesha baadhi ya matukio ya kishujaa aliyo fanya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu, na huduma aliyo mpa ndugu yake imamu Hussein (a.s) na familia yake, ikiwemo tukio la kuwapa maji ya kunywa, filamu hii imetengenezwa katika ufundi na ustadi wa hali ya juu kabisa, imezingatia mambo mengi, ikiwa ni pamoja na historia halisi ya wakati ule, namna ya mazungumzo yao.., hakika ni filamu ambayo imetimiza vigezo vyote vya kua filamu bora ndio maana imeweza kuzishinda filamu zingine zinazo fanana nayo na zilizo tengenezwa na mabingwa wa filamu wa ndani na nje ya Iraq”.
Akaongeza kusema kua: “Hii ni moja ya kazi nyingi zilizofanywa na studio yetu ambayo imepata uzoefu mkubwa katika kazi hizi, pia inaendana na vifaa vya kisasa vinavyo milikiwa na studio, hali kadhalika tuna kitengo maalumu cha picha za katuni”.
Akamaliza kwa kusema kua: “Hakika kufaulu kwetu na kupata zawadi hii, kunatupa moyo zaidi wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha filamu zingine bora zaidi”.