Hivi punde: Kuanza kwa opreshen ya kuulinda mji wa Samara, kikosi cha Abbasi chachukua jukumu la upande wa kusini..

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo Juma Pili (25 Dhulhijjah 1438h) sawa na (17/09/2017m), imeanza rasmi opreshen ya kuulinda mji wa Samara na uwezekano wa kujipenyeza magaidi wa Daesh wakitokea katika maeneo ya Sayyid Ghariib, Farhatiyya na Rafiaat ambao ni upande wa magharibi ya miji ya Balad na Dujail.

Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kimechukua jukumu la kulinda upande wa kusini kikishirikiana na kikosi namba (74) cha jeshi la serikali pamoja na jeshi la anga la Iraq.

Majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) na washirika wao walianza kazi ya msako katika mashamba yaliyopo katika maeneo ya Sayyid Ghariib, yenye misitu mikubwa na uwote mzuri.

Msako huu unaendeshwa na kikosi cha dharura kikishirikiana na jeshi la wilaya ya Dujail, lengo kubwa la msako ni kuhakikisha usalama wa eneo hili baada ya kukumbwa na matukio ya uvunjifu wa amani uliyo tokea mara kwa mara siku za nyuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: