Kikosi cha Abbasi (a.s) kimebainisha kua, katika msako walio endesha upande wa kusini, ambao kikosi namba (74) cha jeshi la serikali kilishirikiana nao, wamepata mafanikio yafuatayo:
- 1- Wamefanya msako katika eneo la kilometa (80).
- 2- Wameangamiza maeneo yaliyo kua yanatumiwa na magaidi ya Daesh.
- 3- Wameteka vifaa vya kurushia makombora ya Haaun katika mji wa Rafiaat.
- 4- Kikosi cha uhandisi kimefanikiwa kutegua mabomu yaliyokua yametegwa aridhini barabarani na katika mashamba ya mji wa Sayyid Ghariib na Balad.
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) umethibitisha kua, miji ya Balad na Dujail itabakia salama na vitendo vya ugaidi, wapiganaji wao wako macho wakati wote na watawanasa magaidi popote watakapo kua.
Kumbuka kua opreshen ya kuulinda mji wa Samara ilianza asubuhi ya leo kwa kushiriki kikosi cha dharura na wanajeshi wa wilaya ya Dujail, lengo kubwa lilikua ni kuhakikisha usalama unarejea katika miji hiyo baada ya kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi katika siku za nyuma.