Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar amesema kua: “Hakika utengenezaji wa mlango wa Hamdu, wa malalo ya Sayyid Muhammad bun imamu Ali Haadi (a.s), chini ya kauli mbiu ya (utengenezaji wa Iraq) tena kwa mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ni dalili nyingine ya uwezo na ubunifu wa watu wa Iraq kua wakipewa fursa na vitendea kazi wanaweza kufanya mambo makubwa”.
Aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa mlango huo ambao umetolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kuipa malalo ya Sayyid Muhammad (a.s), ili uchukue nafasi ya mlango ulio haribika kutokana na shambulio la kigaidi, hafla hii imefanyika katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya cha kutengeneza milango na madilisha ya malalo na mazaru tukufu, katika mkoa wa Karbala, alasiri ra Juma Tatu (26 Dhulhijjah 1438h) sawa na (18 Septemba 2017m).
Akaongeza kusema kua: “Kwa mara nyingine mikono ya watu wa Iraq, wataalamu miongoni mwa watumishi wa Ataba tukufu, wamefanya kazi nzuri sana, hakika wamechagua maneno yafaayo, hati na mapambo, hii ni mara ya kwanza kutengenezwa mlango wa nje wenye sifa kama hizi na kila kitu kimefanywa na raia wa Iraq”.
Akabainisha kua: “Mlango huu umetengenezwa kutokana na agizo la kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, umesanifiwa ma kutengenezwa na Atabatu Abbasiyya kisha umekabidhiwa kwa uongozi wa malalo ya Sayyid Muhammad Sab’u Dujail (a.s), baada ya kutokea shambulizi la kigaidi lililo fanywa na Daesh maadui wa dini na ubinadamu, lililo pelekea kuharibika kwa mlango na kuuawa mazuwaru watukufu pamoja na watumishi wa malalo hiyo takatifu, pamoja na baadhi ya wakazi wa mji wa Balad”.
Akasema: “Ukamilifu wa kazi hii tukufu ambayo leo Atabatu Abbasiyya tunaikabidhi, umetokana na juhudi za ndugu zetu wataalamu wa kiwanda cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi na sehemu tukufu za mazaru, ndugu walio simamia mradi huu katika kamati kuu ya uongozi ni Haji Aadil Jafari Taqiy, Haji Ali Swafaar na kaka Ali Salum, pamoja na wataalamu wa hati, wakiwemo wachoraji na watumishi wote wa kiwanda hiki tunatoa shukrani kubwa sana kwao”.
Akaongeza kua: “Wakati ambao watu wamebeba siraha kukomboa aridhi ya Iraq kutoka katika makucha ya Daesh, wengine wanatengeneza yale yaliyo haribiwa na magaidi hao”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie vitendo vyetu vyema na awalinde maraajii wetu wakuu na atudumishe katika amani”.