Kwa mara ya kwanza tangu miaka tisa: Uongozi wa Zaharaa (a.s) wajiandaa kuonyesha igizo la vita ya Twafu katika aridhi tukufu ya Karbala..

Maoni katika picha
Mapokezi ya mwezi mtukufu wa Muharam, uongozi wa Zaharaa (a.s) chini ya Mawaakibu Husseiniyya (vikundi vya Husseiniyya) katika mkoa wa Diwaniyya wanajiandaa kuonesha igizo la vita ya Twafu kwa mara ya kwanza katika aridhi tukufu ya Karbala katika mwezi wa Muharam (1439h), hapo awali walikua wakionyesha igizo hilo katika mji wa Ghamaas miaka tisa ya nyuma, igizo hilo mwaka huu litaonyeshwa mwezi 12 Muharam 1439h katika barabara ya Najafu – Karbala, kwani siku kumi za kwanza ndani ya mwezi mtukufu wa Muharam ni siku maalumu kwa wakazi wa Karbala kutoa huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara.

Maandalizi ya shughuli ya kuonyesha igizo hilo yamefanyika mbele ya ugeni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mtafiti wa kiislamu dokta Majid Faraju-llah alizungumza kuhusu malengo na misingi ya mapambano ya Imamu Hussein (a.s) na vipi yaliweza kumaliza utawala wa madhwalimu, waliofanya kila jambo linalo pingana na misingi ya maadili ya kibinadamu kwa ajili ya maslahi ya kidunia.

Haji Haadi Atwishaan Shamraan, kiongozi wa kikundi cha Zaharaa (a.s), ameeleza kuhusu maandalizi ya igizo hilo kwa kusema: “Kikundi cha Zaharaa (a.s) kinajiandaa kuonyesha igizo la vita ya Twafu katika aridhi tukufu ya Karbala ndani ya mwezi wa Muharam, ambao lilitokea tukio la kudhulumiwa Imamu Hussein (a.s) na maswahaba zake na hatimae wakafanyiwa waliyo fanyiwa katika siku ya mwezi kumi Muharam mwaka wa 61 hijiriyya.

“Maandalizi yanaendelea kwa miezi sita sasa, tulianza baada ya kupata kibali kutoka katika mkoa mtukufu wa Karbala pamoja na kupewa ruhusa na kitengo cha Mawaakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), tuna andaa mahema na kufanya mazoezi, tumekua tukifanya igizo hili katika mji wa Ghamaas kwa zaidi ya miaka kumi na nne mfululizo, mwaka huu tumeona ni vizuri igizo hili tukafanyia katika aridhi tukufu ya Karbala, aridhi takasifu, aridhi ya shahada na utukufu”.

Muhadhiri wa mimbari ya Husseiniyya Sayyid Ali Abuu Ghanimah, mmoja wa waigizaji wa igizo hili amesema kua: “Hakika idadi ya watu tulio waandaa kama wanajeshi wa ubande wa bani Umayya wanafika (1200), na wapiganaji wa upande wa Imamu Hussein ni kati ya watu (30 – 35) pia kuna kundi la wanawake na watoto”,

Kuhusu maandalizi ya riwaya (maneno) amesema kua: “Hakika riwaya (maneno) yatakayo semwa tumeyafanyia uhakiki kwa wanachuoni na watafiti katika mji mtukufu wa Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: