Maelezo kuhusu bendera tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) itakayo pandishwa katika mwezi mtukufu wa Muharam..

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuupokea mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam, idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri imekamilisha ushonaji wa kitambaa cheusi kitakacho pandishwa katika kubba tukufu usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam mwaka 1439 Hijiriyya, katika hafla maalumu ya kuomboleza ambayo hufanywa kila mwaka.

Maelezo kuhusu wasifu wa bendera hiyo yametolewa na kiongozi wa idara Ustadh Abduzahara Daud Salmaan kua: “Kazi ya kusanifu na kushona bendera inapitia hatua nyingi, kwanza kuchagua kitambaa bora zaidi kitakacho vumilia hali ya hewa bila kuharibika rangi yake, kisha kukadiria vipimo halafu ndio tunaingia katika hatua ya ushonaji, miongoni mwa sifa zake ni:

  • 1- Kitambaa kina ukubwa wa mita tatu na nusu (3.5) upana na kina mita mbili na nyusu (2.5) urefu.
  • 2- Pande mbili zote za bendera zinafanana.
  • 3- Kila upande limeandikwa neno lisemalo: Ewe mnyweshaji wa wenye kiu Karbala (Yaa saaqi atwaasha Karbala), neno hili ni rasmi katika mwezi wa Muharam na Safar peke yake, yameandikwa kwa hati ya Thuluth, tena kwa uandishi wa Ustadh Faraas Asadiy.
  • 4- Ukubwa wa maandishi ni mita moja na senti mita ishirini.
  • 5- Maandishi yote kwa ujumla yanachukua ukubwa wa mita mbili na nusu na yanakua mekundu.
  • 6- Uzito wa pendera ni kilo mbili na nusu takriban.

Kumbuka kua bendera tukufu zinazo wekwa katika kubba –Iwe zile zinazo pepea katika mwezi wa Muharam na Safar au katika miezi mingine ya mwaka- hubadilishwa kila baada ya siku kumi, sawa na bendera tatu kila mwezi, hii ni kutokana na mazingira ya hali ya hewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: